Chungu Anayoipata Waziri Nyalandu Hata Kaa Aisahau

MACHUNGU wanayokutana nayo mawaziri wanaopewa kuiongoza Wizara ya Maliasili na Utalii, siyatofautishi na yale yatajwayo kupatikana jehanamu mahali kunakotajwa kuwa ni kwenye mateso ya watenda dhambi.

Alipoteuliwa Waziri Lazaro Nyalandu kuongoza wizara hiyo niliyoibatiza jina baya, nilistaajabu kumuona akiwa mwenye furaha kana kwamba aendako kulikuwa ni mahali pema. Jehanamu ni jehanamu tu, nia aliyoiita njema ya kuwaondoa vigogo wa wanyamapori, Mkurugenzi Alexander Songorwa na msaidizi wake Jaffer Kidegesho kama njia ya kutekeleza azimio la bunge na kusafisha ufisadi, duru ziligeuzwa na kuwa ubaya.

Kelele zikasikika kuwa, kitendo cha kuwasimamisha watumishi hao ilikuwa ni njia ya kujisafishia ulaji rahisi, kwamba amewatoa wachapakazi ili iwe rahisi kwake kujisevia maliasili.

Kwa kuwa chemichemi ya maji machungu haiwezi kutoa maji matamu, Katibu mkuu wa wizara hiyo Maimuna Tarishi aliibuka, sijui kwa kutumwa na nani, akawarejesha vigogo waliofukuzwa na Nyalandu, huku Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue akimfedhehesha waziri huyo kwa kumwambia hakufuata sheria, kanuni na taratibu za kumfukuza mtu kazi.

Swali langu; kama Nyalandu hajui hata sheria ndogo kama hizo alikuwa na sifa gani za ziada kuteuliwa kuongoza wizara hiyo nyeti? Narudi kulekule nikowahi kusema, mfumo wetu wa utawala una walakini!
Waziri Nyalandu anakuwa waziri wa 11 kupwaya kwenye wizara hiyo ndani ya miaka michache.

Najipongeza kwa jina kwamba maliasili ni wizara yenye sifa za jehanamu kwani hakuna waziri aliyewahi kuiongoza kwa mafanikio na furaha, kila aliyekuja alinusa kwa miaka miwili na kuondoka zake kwa aibu, kidogo Zakhia Meghji ambaye alikaa kwa miaka saba na kisha kisa cha uuzwaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, kikamuondoa.

Mwaka 1988-1990, Waziri Arcado Ntagazwa aliongoza wizara ya maliasili, viatu vikampwaya, akalaumiwa sana kwa ufisadi kwamba alibinafsisha hoteli za kitalii kiholela ikiwemo Lake Manyara, Ngorongoro, Seronera na Lobo.

Ntagazwa alipotimuliwa ‘jehanamu,’ akaingia Abubakari Mgumia, 1990-1993, akaambiwa ameshindwa kudhibiti uharibifu mkubwa wa misitu kutokana na kushamiri kwa biashara ya mbao.
Alipotokomezwa Mgumia, akaingia Juma Hamad Omar, huyu akakumbwa na kashfa nzito kupata kutokea ya kuliuza Pori la Loliondo, akafukuzwa kwa aibu kubwa.

Baadaye 1995-1997, ‘jehanamu’ ikamwita Juma Ngasongwa, naye hakufaa, biashara ya uuzaji wa minofu ya samaki nje ya nchi bila kibali ikamwondoa na nafasi yake kushikwa na Meghji 1997-2005.
Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete ikaanza na Anthony Diallo, akadumu kwa miaka miwili, mvutano kati yake na watendaji wa wizara na kashfa ya uuzwaji wa vitalu, vikamng’oa na nafasi yake kuchukuliwa na Profesa Jumanne Maghembe, ambaye maji yalizidi unga akatolewa ndani ya mwaka mmoja tu, 2007-2008, kwa kushindwa kusimamia vema uuzwaji wa vitalu na uvunaji miti.

Uteuzi ukamfuata Shamsa Mwangunga, 2008-2010, mambo yakamshinda akatolewa kwa kashfa ya kuongeza muda wa umiliki wa vitalu bila kufuata sheria, nafasi yake ikachukuliwa na Ezekiel Maige, waziri kijana ambaye alidumu kwa miaka miwili kabla ya kuingia kwenye skendo ya kuuza wanyamapori hai kiholela.

Aliposhindwa Maige, akaingia Balozi Khamis Kagasheki, waziri mchapakazi aliyeaminika na kila mtu, akafanyiwa mizengwe kwa kuhusishwa na Oparesheni Tokomeza, ikamlazimu ajivue gamba na kumwachia msaidizi wake Nyalandu ambaye leo anatajwa kuwa hajui hata sheria za uajiri. Pole Nyalandu ‘jehanamu’  hakuna furaha. Nachochea tu!
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. unamsifia sifia nyalandu wakati na yeye ni muza pembe za ndovu maarufu

    ReplyDelete
  2. nimesoma kidogo hbr hapo juu nadhan hauko aware na yanayoendelea maliasili.huwezi kujiuliza miaka yote iyo migogoro ipo kati ya waziri vs wakurugenzi na makatibu wakuu?simple answer"waziri ni mtendaji wa serekali bt anawajibika political legitamacy kutetea nafasi yake kisiasa but mkurugenzi wanawajibika legal legitamacy" ndo chanzo cha kutofautiana.pia someni sheria za utumishi wa umma.nyalandu amejifedheesha mwenyewe maana hata kama hajui kusoma hata picha haoni huko nyuma ya akina dialo na severe.

    ReplyDelete
  3. Ma-ccm yameshindwa kuongoza kila KITU kwa ufisadi wao,kama ni kweli katibu mkuu wake Kinana ni muuza pembe za ndovu unategemea nini?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli hapo lazima kazi inakuwa ngumu cos mabosi wako ndio vinara wakuu wa kunya mavi kama sio uharo hapo maliasiri!rais ambae ndio bos wako mkuu aliye kuteua ameshindwa kama sio kuwaogopa mafisadi na majangili itakuwa wewe uharo tu kwao!pole yako.

      Delete
  4. SOFA nzuri inauzwa hadi 13M.... na zinanunuliwa kama karanga... unategemea ni watu wa aina gani wanaomudu kununua kama si wauza PEMBE na wauza SEMBE..... sasa jaribu kuiwazuia ukioneeeeeee....

    ReplyDelete
  5. swali langu ni kuwa ni kwa nini nyalandu hakumchukua mr songrwa wakati alivyo safari kwenda kwenye mkutano wa wanyamapori mjini London? uoni kuwa alimzunguka mkurungezi na baada ya kutoka London akawafukuza kazi hii si sahii kabisa ,nyalandu muogope mungu na omba mungu akusamehe ulichowafanyia hawa jamaa.nyalandu mie nakufahamu sana toka Enzi za school ilboru. umefanya makosa itabidi wewe uwajibike kwa manufaa ya taifa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad