Daktari Anane na Kusema Kuambiana Amejiua

IMEVUJA! Siku chache baada ya kifo cha mwongozaji na mwigizaji wa filamu Bongo, Adam Philip Kuambiana, daktari mkubwa wa mastaa ameibuka na kudai marehemu alijiua mwenyewe.

Kwa mujibu wa daktari huyo ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini kutokana na maadili ya taaluma yao kuficha siri ya mgonjwa, siku moja kabla ya kifo (Ijumaa ya Mei 16, mwaka huu), marehemu alimpigia simu na kumwambia amekunywa dawa za malaria aina ya Fansidar lakini pia amekunywa pombe.

ILIVYOKUWA
Daktari huyo alieleza kuwa, marehemu alimpigia simu kumuomba ushauri juu ya nini cha kufanya na kama kuna madhara yoyote juu ya pombe hizo na dawa alizokunywa.

“Aliniuliza kama kuna madhara yoyote ambayo anaweza kuyapata kwa kuwa alikuwa amekunywa fansidar kwa ajili ya malaria kisha akapata kiu ya bia na kuamua kunywa,” alisema daktari huyo.

AMSHAURI KWENDA HOSPITALI
Akizidi kuzungumzia tukio hilo, daktari alikwenda mbele kwa kusema licha ya msanii huyo kuwa na ‘masikhala’ mara kwa mara, lakini kwa kuwa alimwambia jambo ambalo linahusu uhai wake, alimshauri kwenda hospitali iliyo karibu ili akaonane na daktari kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kutoa sumu kwani kitaalam mtu anapokunywa pombe akiwa amemeza dawa za aina hiyo vyote hugeuka kuwa sumu.

Alisema kutokana na jinsi alivyozidi kumsimulia hali aliyonayo, aliamini kwamba marehemu alikuwa anamaanisha alichokuwa akikisema hivyo ikabidi amsisitize kuwahi hospitali haraka.

“Nilimwambia awahi hospitalini haraka kwani nilijua fansidar ni kali na si dawa ya kufanyia mchezo. Lakini kesho yake nilipopata taarifa za kifo chake niliumia sana japokuwa nilijua amejiua kwa kuchangaya fansidar na bia maana mchanganyiko wa sumu yake mwilini ni mkali sana,” alisema daktari huyo huku akisisitiza kusitiriwa kwa jina lake.

MAZINGIRA YA KIFO
Kwa mujibu wa mtu ambaye alikuwa karibu na Kuambiana siku ya tukio ambaye naye hakutaka kutajwa jina gazetini, marehemu asingekufa ghafla kama tatizo alilokuwa nalo lingekuwa la vidonda vya tumbo ambavyo vilikuwa vikimsumbua kwa muda mrefu.

“Siku ile marehemu alikuwa na pesa, alikunywa sana pombe kutoka asubuhi mpaka usiku mwingi, alikuwa anakula kila anapojisikia sasa hatuelewi ni kitu gani kilitokea maana haiwezekani mtu akutwe anaendesha na kutapika damu pasipo kuwa na sumu mwilini,” alisema mtu huyo.

DAKTARI AWAASA MASTAA
Katika hatua nyingine, daktari huyo aliwashauri mastaa wengine kuwa makini kwani mara kadhaa amepata kesi za namna hiyo ambapo wanakunywa pombe vilabuni usiku huku wakiwa katika dozi ya ugonjwa fulani.
Source:GPL

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mimi nafikiri wawe wanalazwa! hata kama wanaumwa uggonjwa mdogo tu! tuwafungie!

    ReplyDelete
  2. mdao kweli hiyo ndio sululu maana Tz tutawapoteza wengi Rest in peace kau

    ReplyDelete
  3. muache kunywa dawa na pombe... Ushaur wa dokta muufate

    ReplyDelete
  4. sijapata kuona mtu anaendekeza pombe kushinda uhai wake

    ReplyDelete
  5. Tatizo wasani wapenda starehe,wanasema kafia kazini sasa kama wanafanya kazi wamelewa sana ya Bongo haiwezi kupanda

    ReplyDelete
  6. siku moja kabla Marehemu hajafa alikua na pesa nyingi sana. cha ajabu alipokutwa chumbani kwake hakua hata na cent mfukoni.

    ReplyDelete
  7. Hee hakuwa na hela!

    ReplyDelete
  8. huu ni uzushi na mengi yataongelewa sana kuhusu kifo cha huyu jamaa ila km kweli mgeona take one ya zamaradi week hii ndio mgeamini huyu jamaa alikuwa anaumwa kweli na hiyi ilikuwa ni mwezi uliokwisha walikuwa location wakishoot video ya mtitu ni kweli baadhi ya sin zilikuwa zinamshinda kuendelea kushoot mpk anakatisha anaenda pembeni kupumzika then anarudi kuendelea ni wazi kweli alikuwa anaumwa huku akiendelea na kazi muda anapumzika anawaambia wenzake naumwa niombeeni lkn kwakua alikuwa mtu wa matani sn walishindwa kuamini kweli anaumwa mpk aliposhindwa kabisa kuendelea kumalizia sin yake na kupelekwa hospital na sin zake kumaliziwa na mtitu akaja akatoka hospital na kuweka kambi kuanza kucheza movie yake binafsi end of the day akazidiwa na kifo kikamkuta akiwa akishoot movie yake mwenyewe sasa hapo sumu kanywa muda gani?kanumba alifariki yalisemwa mengi sana kuhusiana na kifo chake lkn tukumbuke kuwa mungu akipanga cku yako leo utakufa jua utakufa tu kwani hamjawahi kuckia mtu amelala mzima na akakutwa kafariki bila ugonjwa?kila mtu ataondoka ahadi yake ikifika iwe kwa uzima,malazi,ajali,na vinginevyo

    ReplyDelete
  9. sisi wote ni wa mw/mungu na kwake tutarejea ( Kila nafsi Itaonja kifo)

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad