Daktari Asahau Kitambaa Tumboni Wakati Akimfanyia Mzazi Operation..Kizazi Chaoza

MKAZI wa wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Mwamini Adamu ametolewa mfuko wa kizazi na kukatwa sehemu ya utumbo baada ya mganga wa idara ya upasuaji katika wilaya hiyo kusahau kitambaa tumboni kwa mwanamama huyo wakati akijifungua.

Kutokana na kumsababishia ulemavu huo kwa uzembe, Mwamini ameifikisha Halmashauri ya wilaya ya Urambo kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Magharibi akidai fidia ya Sh milioni 500.

Mwamini ambaye anadai kuwa alipwe kiasi hicho cha fedha kutokana na uzembe wa uliofanywa na Dk Jacob Kamanda aliyemfanyia upasuaji wakati wa kujifungua na kumsababishia aondolewe mfuko wa kizazi pamoja na kukatwa utumbo.

Mwamini pamoja na mumewe Idrisa Jafari katika madai yao wametaka walipwe fedha hizo kutokana na makosa ya uzembe uliofanywa na wataalamu wa upasuaji kwa kuacha kitambaa tumboni mwa mama huyo.

Akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji Amir Mruma jana, mama huyo alidai kuwa Januari 6 mwaka 2011 alijifungua kwa upasuaji baada ya hapo hali yake ilizidi kuwa mbaya huku akitokwa usaha ukeni na sehemu ya tumbo kwenye mshono.

Huku akiongozwa na wakili wa kujitegemea Mussa Kwikima, mama huyo aliiambia mahakama kuwa hali hiyo ilifanya apelekwe hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete bila mafanikio ndipo ikamlazimu kwenda Itigi kwa matibabu zaidi.

Katika uchunguzi wa kitaalamu uliofanywa na madaktari bingwa, Haile Sales ambaye ni raia wa Italia pamoja na Anatole Lukonge wa hospitali hiyo ya Itigi, waligundua kuwa kuna kitu tumboni kama uvimbe hivyo wakalazimika kumfanyia upasuaji mwingine.

Baada ya upasuaji huo walikuta kitambaa cha rangi ya kijani ambacho kilikuwa kimeozesha mfuko wa uzazi pamoja na utumbo kugandana na kitambaa hicho ikabidi kitambaa hicho kutolewa na kusababisha kupasuka kwa utumbo ili kumnusuru maisha yake.

Naye daktari bingwa wa magonjwa ya akinamama na ambaye ni mganga mkuu wa hospitali ya Itigi, Anatory Lukonge katika ushahidi wake ameiambia mahakama hiyo kuwa alimpokea mlalamikaji akiwa anatokwa na usaha ukeni na sehemu iliyoshonwa.

Dk Lukonge amebainisha kwamba walipomfanyia upasuaji mama huyo, walikuta utumbo umeshikana na mfuko wa uzazi huku kukiwa na kitambaa kimeng’ang’ania juu yake.

Alisema wakati walipojaribu kukiondoa kitambaa hicho kibofu cha mkojo kilipasuka wakalazimika kumuwekea mpira ili uweze kumsaidia kutolea uchafu.

Kesi hiyo ya madai namba 13/2011 imeahirishwa hadi Agosti tatu mwaka huu itakapoendelea kusikilizwa kwa upande wa utetezi kuleta mashahidi wake.
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni uzembe mkubwa sana dah inasikitisha

    ReplyDelete
  2. Binaadam tunamapunguf hawez kuwa kama mung alikosea tu kwa bahat mbaya mctak utajir kupitia kosa lake

    ReplyDelete
  3. Ndo shule zetu za kukariri bila mazoezi ya kutosha...kuunganisha utumbo na mfuko wa uzazi kunaonyesha mpasuaji hakuwa amebobea vya kutosha...lack of professional and technical capacity
    Ndo maana Kikwete hata panadol anakwenda Marekani au UK

    ReplyDelete
  4. Duuuuh hii ni hatari madaktari kuweni makini sana.

    ReplyDelete
  5. madaktari ni hatari sana mnatuua jaman,... Jakaya nae hatumii akili badala ya kuleta malecture wafundishe madaktari hapa ye ndo anakimbilia nje kunywa panadol

    ReplyDelete
  6. Hv jamani upasuaji si huwa unafanywa na jopo la madaktar hata wasaidizi wanakuwepo kwaajili ya kusaidia kusogeza mikasi, ina maana hao wote hawakuona?

    ReplyDelete
  7. pumbavu we anoy 1:28 yangekukuta ww ucngeobgea huo usenge wako

    ReplyDelete
  8. hao ndo wanaojijali wao lkn c wengine, ndo kina jakaya wanaofata panadol USA

    ReplyDelete
  9. Weeee msenge binaadam hana ukamilifu ndo majibu yako......wazembeee ndo jina lao sahihi.. unajua principal za u doctors ??
    Muhimbili walimpasua mtu kichwa wakat mtu anaumwa got hii ndo akili au matope??

    ReplyDelete
  10. Mi nakana kuwa ni bahati mbaya, ni uzembe mkubwa tena usiokuwa na umakini, kwani utamshonaje mgonjwa kwani huwezi kuona hich kitambaa? ina kera sana huyu anatakiwa avuliwe udaktari kabisa huwezi kusahau kitambaa katika tumbo la mama, wengine mara wamesaha mikasi, wengine sijui nini na kadhalika, kesi hizi ni nyingi na mi naona huyo jaji amhukumu kwenda jela huyo docta na kutoa fidia ya hela aliyoitaka ingawaje hailingani kabisa na uharibu alioufaya kumtoa kizazi mwenzie, ahukumiwe na iwe fundisho kwa madaktari wengine, wamezoea na hawafikishwi katka chombo chochote cha seria, katika kanunu za uuguzi, hutakiwa kubahatisha kitu kwa kuwa unadeal na uhai wa mtu na si makaratasi wala gali useme likiharibika litaenda garage, nimeudhika na kukasirika kwa kuwa hizi kesi ni nyingi sana na kuna kesi moja iliniumiza sana ilipotokea pale tumaini hosp. Dr. kakosea badala ya kumfanyia operesheni ya kichwa kamfanyia ya mguu aliyetakiwa kufanyiwa ya mguu kamfanyia ya kichwa na alipoteza maisha aliyefanyiwa ya kicha ihali hana matatizo ya kichwa inakera sana achukuliwa hatua iwe fundisho kwa madocta wengine

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad