Diamond Aishiwa Maneno Baada ya Kutajwa Kuwania Tuzo za BET (BET Awards 2014)

Mwaka huu unaonekana kuwa mwaka wa mafanikio zaidi kwa Diamond PlatinumZ ambaye anazidi kuongeza ukubwa wa CV yake katika muziki kwa kupanda ngazi na majukwaa ya kimataifa.

Mshindi huyo wa tuzo saba za KTMA2014 ametajwa jana (May 14) kuwania tuzo kubwa duniani zinazotolewa na Black Entertainment Television (BET Awards 2014) katika kipengele cha Best International Act Africa huku wimbo wake wa My Number One ukiwa umemuwezesha zaidi.

“BEST INTERNATIONAL ACT: AFRICA; NUMBER ONE; (TANZANIA) TANZANIAN STAR DIAMOND PLATNUMZ BECAME A GLOBAL FORCE WITH SUCCESS OF HIS HIT ; NUMBER ONE; AND THAT WAVE MAY CONTINUE WITH A WIN FOR BEST INTERNATIONAL ACT: AFRICA.” Waliandika BET kwenye Twitter.

Diamond anashindania tuzo hiyo na Davido, Mafikizolo, Sarkodie, TiwaSavage na Toofan.

Baada ya kutajwa katika kinyang’anyiro hicho, mashabiki na mastaa mbalimbali walimpongeza huku yeye mwenyewe akiwa ameishiwa maneno kwa furaha.

“Dah! am out of words😓.....Asante sana mwenyez mungu baba kwa kuzidi kuufungulia milango mzikiwetu....” Aliandika kwenye Instagram.

Muda mfupi baadae aliwashuhuku mashabiki wake kwa support yao na kuwataka waendelee kumsupport  kwenye tuzo za MTV (MAMA) na KORA huku wakisubiri muda wa kupiga kura BET Awards.

Tuzo za BET zilianzishwa na kituo cha BET mwaka 2001 kwa lengo la kutambua na kusapoti kazi za wasanii wa Marekani wenye asili ya Africa (African American) au wamarekani Weusi katika nyanja zote za burudani.

Hongera Diamond Platinumz!
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Duuh!!miaka yako hii baba watu wote macho juu!! heee we are proud of you!!

    ReplyDelete
  2. diamond nlikuwa ckukubali kiviile ila sasa umenikonga moyo wangu nakukubali!!!we mkali.

    ReplyDelete
  3. umetoboa mbaya..,,and yet kuna wajeul wachache..,make them knw u...,,God blec u

    ReplyDelete
  4. wakuache ulaleee, cc kazi yetu moja tu kupiga kura, tuachen chuki tumpigie kura jamaa

    ReplyDelete
  5. Tuzo kubaki tz-tanzania inawezekana mungu jalia ibaki si kwa Diamond tu nikwa Tz na Africa kuukubali mziki wa hap om.

    ReplyDelete
  6. hata wakenya mumpigie platinum pamoja waganda maana ndo kachaguliwa kwa east african nzima ni yeye tu

    ReplyDelete
  7. This is Man.....He'z number 1 Tz.......umetufikisha mbali sana DIMOND.....INSHA ALLAH Utachukuwa Award....

    ReplyDelete
  8. X A f xana kaka_ _let us vote u_

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad