Gabo ni Mchaga Au Mmakonde au Ni Teja? Fahamu Hapa

ANASTAHILI kuitwa staa kulingana na uwezo wake  kisanii. Anapaswa kuambiwa anaweza kwa namna anavyoweza kuvaa uhusika kwenye sinema anazoshiriki lakini ni haki akijulikana kwa jina la msanii kwa sababu hachagui uhusika kwenye filamu.

Anaitwa Gabo Zigamba lakini jina alilopewa na wazazi wake ni Salim Ahmed, mume wa Fatmah na baba wa watoto wawili – Salha na Athuman.
Gabo anajua kuvaa uhusika, kubadilika kulingana na hadithi na haoni haya hata pale anapotakiwa kucheza kama teja au kichaa. Kati ya sinema zilizompaisha zaidi ni pamoja na Jicho Langu, Elimu Mtaani, Ukurasa Mpya, Danija, Bado Natafuta, Safari, Majanga na Fikra Zangu.
Katika Exclusive Interview, Gabo amezungumza mengi kuhusiana na sanaa ya filamu za Kibongo na maisha yake kwa jumla.

UNAKUTANA NA CHANGAMOTO GANI?
Changamoto ni nyingi sana lakini kubwa zaidi ni malipo duni kulingana na ukubwa wa kazi tunayofanya.
Wasanii wengi wanapoulizwa kuhusu malipo husema ni mazuri na sanaa inalipa, si kweli.
Wasanii tunaumia sana, wengi hawapendi kuwa wakweli. Kwa sasa wanaonufaika ni watayarishaji na wasambazaji.

UMEPATA MAFANIKIO GANI KUTOKANA NA SANAA?
Namshukuru Mungu, kiasi mambo yanakwenda sawa. Nimejenga nyumba yangu, silipi kodi lakini kujulikana pia kunanisaidia mengi.
Unajua ukishakuwa na jina, basi huduma nyingi za kijamii unazipata kwa wakati na kwa thamani ya kistaa. Hilo linalinifurahisha.


KITU GANI KIZURI USICHOWEZA KUKISAHAU?
Siwezi kusahau siku ambayo mke wangu alinipatia mtoto wangu wa kwanza Salha. Ilikuwa siku ya kipekee maana tulikaa muda mrefu sana bila kupata mtoto.

Kama unavyojua tena, tayari waswahili walishaanza kusema yao. Ikawa kama tumewaziba mdomo. Ilikuwa siku yenye furaha na ya kukumbukwa maishani mwangu.
Ili kuonesha furaha yangu, kila script (mwongozo wa hadithi) ninayoandika huwa natumia jina la mwanangu Salha.


KWENYE MATUKIO YA KISANII, NINI HAKIWEZI KUFUTIKA KICHWANI MWAKO?
Ilikuwa Mbezi (Dar) tukiwa location. Tulikuwa tunarekodi filamu ambayo hapa naomba nisiitaje, sasa kuna dada ambaye ndiye alikuwa mhusika mkuu.
Jamaa yake (mpenzi) alikuwa anakuja mara kwa mara pale location. Kuna siku wakagombana, jamaa akaondoka akiwa amekasirika. Siku iliyofuata asubuhi, tukashangaa yule dada akiwa amefariki.
Shooting (shughuli za kurekodi) ikaishia hapo na mpaka leo ile sinema haikutoka. Kiukweli hilo ni tukio ambalo halijawahi kutoka akilini mwangu kabisa.


UNAONEKANA KUPATIA SANA KUIGIZA UTEJA, VIPI ULISHAPITIA HUKO?
Sijawahi na sifikirii kufanya hivyo. Mimi kama msanii natakiwa kuvaa uhusika wa namna yoyote ile. Sioni vibaya maana pale nakuwa namwakilisha mtu mwingine.
Kuna sinema nyingine nimetumia lafudhi ya Kimakonde mfano kwenye Bado Natafuta na Fikra Zangu, ukiangalia Danija nimezungumza kama Mchaga. Kuna watu wanafikiri labda natokea kwenye moja ya makabila hayo.
Si kweli, mimi asili yangu ni Tanga kwa upande wa baba na mama ni Iringa. Ni usanii tu, hakuna cha zaidi.

KUNA TOFAUTI GANI YA SOKO ENZI ZA UHAI WA MAREHEMU KANUMBA NA SASA?
Steven Kanumba alikuwa akijitambua, yule bwana alikuwa na uwezo wa kipekee. Ni kweli kuwa alisaidia sana kukuza soko na ushindani. Baada ya kifo chake naweza kusema mwamko wa soko umepungua kidogo.
Juhudi zaidi zinahitajika. Lazima watu wawe na ubunifu na kiu ya kupaa kimataifa kama ilivyo kwa Kanumba, siyo kuridhika na mahali tulipo. Tukifanya hivyo tutafika mbali.

UNAZUNGUMZIAJE USHIRIKINA KWENYE FILAMU?
Uchawi upo, nasikia kuna watu wanalogana na wengine wanatumia dawa ili wang’ae lakini kwa upande wangu namwamini Mungu. Najua akipanga, amepanga, hakuna wa kupangua.

SKENDO KWA WASANII VIPI?
Msanii akifanya kitu kinyume na kazi yake anaharibu. Mimi ninachokiona ni matumizi mabaya ya akili. Kama unaheshimu sanaa kama kazi, ni wazi kuwa utakaa mbali na skendo.

UNA MATARAJIO GANI?
Kwa sasa nimejipanga kuanza kutayarisha sinema zangu mwenyewe, naamini hapo utakuwa mwanzo wa mafanikio yangu. Nimeanza kujipanga vizuri, muda si mrefu nitaingia mwenyewe kama Gabo Zigamba.

UNAMZUNGUMZIAJE MAREHEMU KUAMBIANA?
Kama Adam (Kuambiana) alikuwa jembe. Alikuwa na vitu vikubwa viwili, kwanza elimu ya uongozaji na msimamo. Alikuwa hapendi kuyumbishwa. Tulipanga kufanya mambo mengi sana pamoja lakini ndiyo hivyo, Mungu amemchukua.

Kifo chake kilinishtua sana, ingawa nilikuwa nimelazwa, lakini niliomba kupelekwa hadi Leaders (viwanjani – Kinondoni) kutoa heshima zangu za mwisho kisha nikarudishwa wodini.

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu jamaa(Gabo) kipaji kipo!!nakukubali xana bro!!keep it up..

    ReplyDelete
  2. ana kipaji lkn afaamiki kiiiivo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tv kwenu mnayo kwanza wewe si adi uende kwa jirani ukaangalie utamfahamu vipi sasa

      Delete
  3. huyo jamaa anajua kuna yeye na jb.wako mbali sana kisanaa

    ReplyDelete
  4. Anafahamika sana.. we ndo humjui

    ReplyDelete
  5. angefaamika ningeuliza?

    ReplyDelete
  6. hata mimi cmjui, nahisi anafanya promotion ili ajulikane. kaona aanzie kwenye umbea wa udaku. ila una bahati mbaya make hatukujui, pole.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Angalia bado natafuta, jicho langu au elimu mitaani. Na ujifunze kufatilia sanaa za tanzania kwa kuzinunua na sio kufatilia magazetini. Sasa ev kla msanii mkubwa anampa role kubwa jamaa kwenye movie zake. Kama himfaham it means sio mfatiliaji wa sanaa bali ni msomaji wa magazet ya udaku ambapo wasanii kama hawa wanajioheshm hawawez kutokea...

      Delete
  7. Mcyo fatilia xnaa ndo amu mjui achen majung mbwa nyie GABO anajulikan achen uxng ki2 hujui kaush mnataka xfa nyk zenu ngurue poli.

    ReplyDelete
  8. NAMJUA JAMAA YUKO POA SANA KIZURI TUKIPE SIFA ZAKE AU MPAKA? AFE WABONGO BANA

    ReplyDelete
  9. Hao ni machoko tanzania nzima itakuwa ni wao tuu wawili ndio awamjui waambie wazazi wenu au mabbwana au wake zenu wawanunulie tv mbwa nyie

    ReplyDelete
  10. Kaka mkali sana,na sio LAZIMA wote kumpenda ila Hakuna kama gabo zigamba,baada ya KANUMBA ni gabo na jb

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad