Kama alivyoandikika Edson Kamukana katika makala yake moja "ukiachilia mbali wasomi kadhaa walioamua kulamba matapishi yao na kumtusi Jaji Warioba na wana-CCM wengi wanaotukana bila kujua wanamtusi nani, katikati yake utaona wanaosalia si bure wana jambo na sababu za kufanya hivyo, hawa bila shaka wanalipa kisasi."
Mnamo tarehe Julai 17, 1997, Rais Mkapa alimteua Jaji Warioba kuongoza Tume ya Rais (Warioba Commission) kuchunguza na kubainisha mianya na vyanzo vikuu vya rushwa nchini. Baada ya kufanya mapitio ya sheria, kanuni na taratibu ndani ya serikali na kuonyesha mianya ya kukua na kuongezeka kwa rushwa nchini, Tume ya Warioba ilichapisha ripoti yake (Ripoti ya Warioba) tarehe 7 December 1997.
Baadhi ya mambo ambayo Tume ya Warioba iliyakuta ni pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa umma kuchukua rushwa kama sehemu ya kujazia mishahara yao (petty corruption) midogo. Lakini pia Tume ya Warioba ilikuta kuwa kulikuwa na rushwa nyingine (grand corruption) aka ufisadi iliyohusisha maafisa wa ngazi za juu na baadhi ya wafanyakazi wa serikali walio na ulafi wa kujilimbikizia mali.
Tume ya Warioba ilitoa mapendekezo ya hali ya juu yaliyogusa wizara na idara zote za serikali. Ripoti ya Warioba iligusa mioyo ya walalahoi na wengi waliotoa maoni ya kumtaka Rais Mkapa awafikishe mahakamani wale wote waliohusishwa na ufisadi kwenye Ripoti ya Warioba. Hata hivyo, ripotii hiyo iliwekwa kabatini na kutiwa kofuli. Ripoti ya Warioba ni imekuwa adimu sana kupatika ilivyokuwa kwa Hati ya Muungano.
Japokuwa ripoti hiyo iliwekwa kabatini, iliwagusa moja kwa moja vigogo kadhaa hasa wa CCM na wengi wao au watoto, ndugu na jamaa zao ndio wanaoshika madaraka leo. Kama mnakumbuka baada ya ile ripoti, ndipo vyombo vya habari vilianza kuripoti masuala ya rushwa, ikiwemo ile skendo ya IPTL iliyomfanya Mwalimu Nyerere aseme kuwa "kama huu ndiyo ushirikiano wa nchi za kusini, basi bora ukoloni urudi." Waliounga mkono au kuipinga IPTL wanajulikana. Wengine mtakuwa mnawakumbuka hata watawala wa miaka hiyo na wizara/idara walizokuwa wanaziongoza.
Akihojiwa na gazeti la Raia Mwema Mei 13, 2008, Jaji Warioba alisema kuwa "Baadhi yetu tumepiga kelele muda mrefu kuhusu hali ya rushwa nchini mpaka ikafika mahali ikawa watu wanatoa dhihaka tu. Kuna rafiki yangu mmoja, yeye alinipachika jina la ‘Bwana Kero’ kwa sababu ya taarifa ile ya Tume ya Kero ya Rushwa. Alisema mimi nimegeuka kuwa kero kwa kuzungumzia rushwa kila wakati." Bado anaendelelea kuwa "Bwana kero" kwa kutetea Rasimu ya Katiba Mpya.
Kama alivyouliza Edson Kamukana, inawezekana kweli hao vigogo au watoto wao, ndugu na jamaa zao walioguzwa moja kwa moja na ile ripoti wakamsifu "Bwana Kero" wakati alishawaharibia kitumbua chao? Hatuoni vigogo hao wanautumia mchakato mzima wa Katiba mpya kama mwanya pekee was kumdhoofisha "Bwana Kero" na kujaribu kuendelea kuficha madhambi yao yaliyoyafichuliwa na "Bwana Kero" kwenye ile ripoti yake ya kero za rushwa 1997?
Kwa wale ambao hawakuwahi kuisoma Ripoti ya "Bwana Kero" itafuteni muisome halafu muone "kero" ambazo "Bwana Kero" aliziodhoresha kwenye ripoti yake. Halafu muunganishe the dots kwa kujiuliza ni kwa nini kigogo A na B au mtoto/ndugu/jamaa wa Kigogo C "anakereka" sana mpaka kumtusi "Bwana Kero"? Mara ya mwisho nilisoma muhtasari wa ripoti kwenye maktaba ya HakiElimu. Ilikuwa imejaa vumbi kweli kweli. Inaitwa "The Report of the Presidential Commission of Inquiry Against Corruption", kwa kifupi "The Warioba Report".
Bahati mbaya umesema report yenyewe imefungiwa kwenye makabati. Natamani kuisoma nipate picha halisi nikikingakisha na report ya tume. Inaelekea baadhi ya watoto wa vigogo unaosema sasa ni vigogo wa serikalini.
ReplyDeletenisaidie iyo riport nitaipata wap? Kumbe ndio maana yule dogo analalama alafu najiuliza iyo jeuri kaipata wap? Alafu simpendi ngoja huu mwaka uishe labda jeuri itapungua, alafu bongo watu wanafiki sana ona wanavyojipendekeza hadi kampeni walimpigia, SEMBE + #
ReplyDelete