Kuna kilio kinasikika kwa mbaaali. Wanamuziki na wadau wanalalamika kuwa muziki wa Nigeria unapandishwa na Bongo Fleva inapotezewa.
Cha kujiuliza ni iwapo muziki huu unabebwa au ni ubora wa kazi hizo ndio unaowavutia mashabiki.
Mdj wanajua ili watu wasiondoke katika “dancefloor’’ ni lazima wapige nyimbo za Nigeria. Bila kupiga Testmoney, Ayee, Skelewi, Away Dance, Ginger, Mama Africa, Adama na nyingine usiku wa mpenda burudani hauwezi kuwa umekamilika.
Ukweli ni kwamba hawa jamaa wameshaharibu fomesheni ndiyo maana sasa hivi wasanii wanabuni mbinu mbalimbali ili angalau waweze kupata kitu kidogo.
Kuwakwepa na kutafuta njia nyingine siyo dawa, kinachotakiwa ni kuhakikisha Bongo Fleva inasimama na huu ugonjwa wa ‘Naija Muziki’ unatokomea katika mlango ulioingilia.
Kuna tukio la hivi karibuni limetokea kwenye burudani ya Muziki. Mwanamuziki Davido alipotembelea nchini mwaka jana huenda alituibia kitu na sasa ndicho kinamfanya akombe mamilioni ya pesa.
Inawezekana Davido alipokuja alikusanya CD nyingi za kundi la Offside Trick kama siyo za AT na kwenda kutoka na wimbo mkali ambao sasa unafanya vizuri.
Ukisikiliza wimbo wake, “Aye” una kila sababu ya kuamini kuwa Davido ameiba mahadhi ya mduara wetu na kwenda kufanya mambo mbele ya safari.
Huu ndio ukweli
Bongo Fleva haipo dukani halikadhalika muziki wa Nigeria. Maana yake ni kwamba hakuna duka lolote sasa hivi linalouza cd za muziki. Nyimbo zote unazozisikia mitaani ni za kunyonya kutoka mtandaoni.
Kuwezeshwa kwa mitandao kumeifanya dunia iwe kijiji. Leo hii huwezi kumdanganya mpenda burudani kuhusu wimbo mpya au sinema mpya iliyotoka. Ukifumba na kufumbua utakuta tayari anayo; iwe kwenye simu, kompyuta au cd.
Kwa maana hii kumlaumu mtu fulani kuwa ndiye chanzo cha muziki huu kushika nchini hoja hii haitakuwa na ukweli wowote.
Hatari Tupu:Wanaigeria wanalitibua soko la muziki Bongo
3
May 05, 2014
Tags
Mage wangu ni mzuri
ReplyDeleteacha usenge
ReplyDeleteWakati mwingine hilo huchangiwa na wanamuziki wa bongo fleva wenyewe; hasa wale maaraufu. Kwa mfano ili Diamond atoke kimataifa ilimlazimu amtafute Mnaigeria ndiye awe mwimabji mkuu wa wimbo wake; na akaimba katika kinigeria kabisa. Sasa hata kama wimbo ni wa Diamond ndio unaopata umaarufu, unakuta kuwa umaarufu huo ni kwa sababu ya uimbaji wa Mnigeria. Kwa sasa hivi nadhani ule wimbo original wa diamond haujulikani tena bali ule wa remix na Davido. Kwenye ile performance ya Mtwara, Diamond ndiye aliyekuwa akiiga sauti ya Davido ili kuimba wimbo wa Diamond!
ReplyDelete