Kaka wa Mtoto Aliyefungiwa Kwenye Boksi naye ‘Apotea’

Zimeibuka taarifa kwamba mtoto aliyekuwa amefungiwa kwenye boksi kwa miaka minne na mama yake mkubwa, Nasra Rashid (4) alikuwa na kaka aliyefahamika kwa jina la Nasoro ambaye hadi sasa hajulikani mahali halipo.

Wakati polisi ikisema imefurahi kupata taarifa hizo na kwamba itazifanyia kazi, habari zilizopatikana jana kuhusu hali ya Nasra zimesema atafanyiwa vipimo 18 ili kubaini hali ya afya yake. Vipimo vya awali, vimebaini kuwa amevunjika mifupa ya mikono na miguu na kwamba atapelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Kuhusu kaka yake, baadhi ya majirani wa nyumba aliyokuwa anaishi mama mzazi wa Nasra enzi za uhai wake walidai kuwa Mariamu alikabidhiwa watoto wawili kuwalea baada ya mama yao kufariki dunia.

Mmoja wa majirani hao, Ramadhani Mansuri alisema wakati mama mzazi wa Nasra akiishi eneo la Mjimpya alikuwa na watoto wawili akiwamo Nasoro ambaye aliachwa akiwa na umri kati ya miaka 14-15.

Vipimo

Ofisa Ustawi wa Jamii, Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungamtitu alisema taarifa alizopata kutoka kwa madaktari zinasema kuwa mtoto huyo atafanyiwa vipimo 18 ili kubaini hali ya afya yake.

Akizungumzia matokeo ya vipimo vya awali, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Dk Rita Lyamuya alisema haijafahamika sababu za kuvunjika kwa mifupa hiyo.

Dk Lyamuya alisema jana kwamba, mtoto huyo ameshafanyiwa vipimo vingine kadhaa ambavyo vinaonyesha kwamba anasumbuliwa na homa ya mapafu (pneumonia) na utapiamlo unatokana na kukosa lishe bora.

“Tulilazimika kumfanyia vipimo hivyo vya awali kwa sababu alikuwa anaonekana kama anayeugulia maumivu, kwa hiyo vipimo vingine vitaendelea kufanywa kadri tutakavyoona inahitajika,” alisema Dk Lyamuya.

Alisema kipimo cha X- Ray ndicho kilichoonyesha kuvunjika kwa mifupa yake ya miguu na mikono na kwamba hali hiyo ndiyo inayosababisha ashindwe kusimama na kutembea.

“Wakati anafikishwa hapa hospitalini alikuwa amebanwa na kifua na alikuwa anashindwa kupumua vizuri. Ilitulazimu kumwekea mashine ya oksijeni ili imsaidie kupumua, lakini sasa hali yake inaendelea vizuri na tayari tumeondoa mashine, anaendelea na matibabu mengine,” alisema.

Mbali na tiba, Nasra pia alifanyiwa usafi wa mwili wake ambao ulikuwa mchafu kutokana na kutoogeshwa kwa muda mrefu na sasa inaelezwa kuwa yuko kwenye hali ya kuridhisha na wasamaria wema wameanza kujitokeza kumpa misaada ya nguo na chakula.

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dah hyo mama aliemfanyia unyama mtoto huyu ya wezekana ni mchawi maana kwa mwanamke tena aliezaa hwz kuwa na roho mbya na ya knyama kama ya huyo mwanamke

    ReplyDelete
  2. Duniani kunawatu waajabu sana huwezi amini hichikitendo kama kimetokea.mungu msaidie huyu mtt aweze kua kama watt wengine.

    ReplyDelete
  3. Inawezekana kuna wengine wanafanyiwa vitendo kama hivi basi tu haijajulikana.

    ReplyDelete
  4. Huyo mama anastahili kifo.

    ReplyDelete
  5. Mungu msaidie mtt Nasra apata afya njema

    ReplyDelete
  6. uyo mama ni muuaji seriouz na malipo ni hapahapa duniani, maana mungu hamtupi mja wake hatimae kaumbuka

    ReplyDelete
  7. Natamani kulia mungu msaidie mtoto nasra akue vema

    ReplyDelete
  8. Huyu mama ni muuaji sana hana hata uruma...........kweli mungu ni muweza wa yote atakuwa kwa uwezo wa allah

    ReplyDelete
  9. Kunahaja yakuwekwakwenye vyombo vya hbari kiasi chamwezi mmojja ilikilamtu amuone

    ReplyDelete
  10. Huyo mama hana huruma hata kidogo ni muuwaji mkubwa .

    ReplyDelete
  11. Mungu nakuomba mpe afya njema huyu mtoto

    ReplyDelete
  12. Imeniuma sna jamani......yaan mtoto wa ndug yako wa damu unamfanyia kitendo kama hicho da...kweli kuna binadam wanaroho zaidi ya mnyama...Allah mjailie afya njema mtoto Nasra

    ReplyDelete
  13. Huyo mama anatakiwa kunyongwa tu ana roho ya shetani na mwenyezi mungu atamuadhibu, namuombea sana kwa mungu mtoto Nasra apone na awe na afya njema kwa kweli nimelia sana kutokana na habari za huyu mtoto

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad