Kifo cha Meneja wa Ewura Utata Mtupu

Wakati kukiwa na utata wa kifo cha Meneja wa Biashara ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), imebainika kuwa tofauti ya takwimu kati ya mamlaka hiyo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), iliyotolewa kwenye Kamati ya Bunge ya Bajeti ni Sh25 bilioni.

Meneja huyo, Julius Gashaza alikuwa akihudhuria kikao kilichokuwa kikijadili tofauti hiyo bungeni Dodoma na baadaye aliporudi Dar es Salaam akakutwa amejinyonga hotelini huku ikielezwa kuwa alirudi akiwa amejawa hofu na kukosa amani.

Vyanzo vyetu ndani ya kamati hiyo vimeeleza kuwa tofauti iliyobainika katika hesabu za taasisi hizo za Serikali ni lita 11,755,161, ambazo zingeuzwa kwa bei ya sasa ya petroli mkoani Dar es Salaam ya Sh2,200 zingepatikana Sh25.86 bilioni.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, takwimu za TRA zinaonyesha kuwa kati ya Julai 2013 hadi Machi mwaka huu, kiasi cha mafuta kilichoingizwa nchini kilikuwa lita 2,189,240,000 wakati Ewura ilionyesha ni lita 2,177,484,839.

Hata hivyo, baada ya utata huo na Kamati ya Bajeti chini ya Andrew Chenge kuitaka Serikali itoe ufafanuzi wa tofauti hizo, Serikali iliwasilisha taarifa yake Jumapili ikisema takwimu zote ni sawa.

Katika ufafanuzi wake, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema uhakiki wa takwimu hizo ulibaini kuwa zote zilikuwa ‘sahihi’ na kwamba tofauti iliyopo inatokana na upimaji wa mafuta.

Nchemba alikaririwa akisema TRA hupima mafuta kwenye meli mara inapoingia na kukadiria kodi wakati Ewura hupima mafuta yanapopokewa kwenye matanki.

“Kwa kuwa wakati mwingine meli hutumia muda mrefu tangu zinapoingia hadi zinapoteremsha mafuta, sehemu ya mafuta ambayo TRA huhesabu kama yameingizwa katika mwezi mmoja wakati Ewura hupata takwimu za kiasi cha baadhi ya mafuta hayo katika mwezi unaofuata na hiyo ndiyo iliyosababisha kuwapo kwa tofauti hiyo ambayo hata hivyo ni ndogo.”

Kulingana na takwimu hizo, kiasi cha mafuta kilichoonyeshwa na TRA kilikuwa juu kuliko kile kilichoonyeshwa na Ewura na haijajulikana iwapo kutofautiana huko kwa takwimu kuliifanya Serikali kumweka kitimoto Gashaza.

Alikuwa na hofu

Sintofahamu imeendelea kugubika kifo cha Gashaza na sasa imeelezwa kuwa alirudi kutoka Dodoma akiwa amejawa hofu na kukosa amani.

Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi alisema jana kuwa ingawa hakuzungumza na Gashaza baada ya kurudi kutoka Dodoma, taarifa za polisi na kutoka kwa mkewe zinaeleza kuwa alirudi akiwa na hofu na ndiyo sababu ya kuondoka nyumbani kwake na kwenda kulala hotelini.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ataachaje kuwa na hofu wakati alijua wazi kwamba atamalizwa kama marehemu kaka yake ambaye pia alikufa kifo cha utata miaka 20 iliyopita

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inauma jamani yaan amemuacha mama yake kipenzi mke wake mawatoto wake .hasa mama yake alie kua kila kitu kwake kuliko hata hiyo serikar ,saa mim kwaninavyo Amin mungu hataendelea kuvumilia tuteseke na mna hii kama ilivyo kua ktk siku za noa nfivyo itakavyo kua atakapo hatibu mifumo yote ya utawala WA dunia hii

      Delete
  2. Mh!! Makubwa jamani

    ReplyDelete
  3. Mnadiriki kuua hata huyu?Kabisa serikali chini ya chama cha mapinduzi sio hata kidogo!Nani aje awaambie ukweli ndo muutekeleze?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad