KIGOGO USALAMA WA TAIFA AUWAWA KINYAMA DAR

Ofisa mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa nchini Bwana Silvanus Mzeru ameuwawa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha. Mauwaji hayo ambayo taarifa zake zimeibua hofu kubwa, yalitokea jana jioni katika mataa ya barabarani ya karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Habari zinasema mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la kinyama wauwaji hao waliondoka na briefcase ya marehemu huyo ambayo haijajulikani ndani yake ilikuwa na vitu gani.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kabla ya kuuwawa kwa Mzeru watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walirusha risasi kuelekea katika gari yake.

"Baada ya risasi hizo kurindima, Mzeru aliendesha gari lake kwa kasi na kwenda kugonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake na kisha gari lake kutumbukia mtaroni" Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Mashuhuda hao waliongeza kuwa wauwaji wa Mzeru walimfuata katika mtaro na kuumua kabla ya kuondoka na briefcase iliyokuwa kwenye gari.

Chanzo: Tanzanidaima Toleo namba 3436 Uk 3 la leo Alhamisi, Mei 1 2014.

Mytake:

Kama watu wa usalama wa Taifa wanaweza kuuwawa kinyama kiasi hicho, vipi kuhusu raia wa kawaida?! Kama raia wa kawaida wamekuwa wanapigwa risasi na kuuwa kwa mabomu kwenye mikutano ya vyama vya siasa na waliopaswa kulinda usalama wao, Kumbe haina tofauti na watu wa usalama wa Taifa?! Kama usalama wa taifa huwa wanalalamikiwa kwa kuteka na kutesa kama ilivyosemwa kwa Dr Ulimboka, Nani yuko salama?
Last edited by Mohamedi Mtoi; Today at 13:54.

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. watakua ni wao wenyewe wamemuondoa. probably alikuwa na nyaraka nyeti labda zingevuja ingekuwa soo.
    mdau USA

    ReplyDelete
  2. Hizo ninjama zao wenyewe MTU wanje hawezi jua kwenye briefcase kunann? Niwenyewe tu tuuuunde! Tumeeeeeeeeeeeeeeuwaaaaaa!??

    ReplyDelete
  3. Mdau,USA........,Thatz very obvious

    ReplyDelete
  4. For country security we are ready for anything, its better you take one bad grass which could lead to a massive deaths of hundreds.....thats principle around the world even USA, for country matters of security if you bring childish matter ur out.....

    ReplyDelete
  5. It is so sud,sorry for the family and all Tanzania ,but I hope the leaders saw the sign from the begining due to alot of issues happed before this,the only way to solve this problem is to deal with curruption which face our nation in all corner,also to have univesal army to dearl with this issues, thank you,there kill our animals ,now there stating with human being,we have to work up.

    ReplyDelete
  6. yani ni wao wenyewe ndo wamemdedisha siri za serikali mchezo

    ReplyDelete
  7. Hao ni wenyw kwa wenyw dam za watu zitakuja kuwalilia kwa sababu ya uroho wa hela

    ReplyDelete
  8. TUNASEMA USALAMA WA TAIFA, LAKINI SIYO... NI USALAMA WA GENGE LA WAHUNI..
    .C C M M A F I A

    ReplyDelete
  9. Wamemuuua wenyewe.mbona nchi hii ndiozao walimuua sokoine sembuse yeye nawengne wamewadedisha hovyosana.ilanawao watakufa tu kifo kbaya kwani auae kwa upanga.......somsitie shaka mungu niwawote.ua nawe utakufa tena kifo kbaya mpk ushindwe kutizamika surayako.mbonawengi tu wanakufahvyo nafamilia zao hawaagi mait yke ni sbbu yamambo km haya

    ReplyDelete
  10. Bora tujiweke kwa yesu tutakua salama.......ni kawaida nchi za dunia ya tatu usalama ni mdogo sana...kama vile rpc wa mwanza alivyouawa..marehemu kamanda barow....ni mkubwa ktka jeshi la polisi kauawa ndio mipango ya mungu na sometimes inategemea na matendo ya mhusika...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad