Kim Kardashian Akanusha Tetesi Kuwa Wameshafunga Ndoa

Siku chache baada ya kusambaa tetesi kuwa Kanye West na Kim Kardashian tayari wamefunga ndoa yao ya kwanza (kiserikali), mrembo huyo ameamua kusema na kuzikanusha tetesi hizo.

Bibi harusi mtarajiwa ambaye ataonekana kwenye TV akiwa na mumewe Kanye West watakapofunga ndoa rasmi May 24, ameekanusha tetesi hizo kupitia akaunti yake ya Twitter.

Tetetesi ya pili aliyoikanusha ni pamoja na ile inayoaminika sana kuwa ndoa yao itaoneshwa kwenye show maarufu ya familia yake, “Keeping Up With The Kardashian”.

Kim K alikanusha pia kuwepo orodha ya wageni 1600 iliyosemekana kuwa na majina mengi ya watu maarufu akiwemo Lupita Nyong’o, Winnie Mandela na wengine.

Na mwisho akawatahadharisha watu kuhusu picha za nguo zake za harusi zinazosambaa kuwa sio za kweli.

“Seeing fake wedding dress pics of me. No one has seen my dress! Those photos are old or photo shopped.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad