Kinana Amtaka Maalim Seif Ajiuzulu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharif Hamad, kama kweli hataki Muungano wa serikali mbili, amuandikie barua Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein na kujiuzulu wadhifa wake wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Tamko hilo lilitolewa jana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara, uliofanyika kwenye viwanja vya Kibandamaiti mjini Unguja.

Kinana alisema anachokifanya Seif ni sawa na kuwaramba vichogo wanasiasa wenzake wa upinzani, wakati yeye akipata mshahara na marupurupu mengine, yanayomwendeshea maisha yake chini ya serikali ya CCM.

Alisema kama kweli Maalim Seif anajigamba ni jasiri, achukue uamuzi sahihi wa kujiuzulu wadhifa wake, ili apate nafasi ya kutosha kuwatumikia wananchi nje ya Serikali.

Kinana alieleza kuwa kutembea nchi nzima kwa Seif, si kitendo cha uungwana kufanywa na kiongozi mwenye wadhifa wa Makamu wa Kwanza wa Rais, akiwa ndani ya Serikali inayomlipa mshahara na huduma nyingine muhimu, akaamua kuwachochea wenzake, ambao wako nje ya Serikali kuleta chokochoko dhidi ya Serikali anayoitumikia.

Maalim Seif ameshatuhumiwa kuwa kigeugeu katika maisha yake ya kisiasa, ambapo hivi karibuni Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Mohammed Seif Khatib, alielezea namna kiongozi huyo wa CUF, alivyowahi kuwa mtetezi wa serikali mbili alipokuwa kiongozi katika Serikali ya CCM, ambako alitumia nguvu kubwa kupinga vuguvugu la kudai serikali tatu mwaka 1984.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Toka awe makamu wa kwanza wa rais hata kanzu havai dawa yake kuondoa serikali ya mseto ale jeuri yake

    ReplyDelete
  2. Seifu ana kazi kubwa kula mshahara wa unafik.....kuchochea vurugu yeye anakula bata...mwaka 1984.....na mwaka 1995...ambao huo mshahara utamchoma....manake mpaka mauaji yalitokea sema uongozi wa ccm una busara sana..

    ReplyDelete
  3. bongo watu wanafiki sana sio huyo tu wapo kibao tena ccm ndo kibao

    ReplyDelete
  4. Kinana kujigamba kwamba Seif analipwa na CCM, unafiki mkubwa, hizo ni pesa za wananchi sio CCM

    ReplyDelete
  5. Ndio maana kinena anatumia pesa za serikali akidhani ni za ccm .mfunuweni macho huyu ana usingizi mzito .Bado anadhani upo mfumo ule uleee wa chama ni baba ni mama

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad