Kocha wa kwanza mwanamke kufundisha soka kwenye klabu kubwa Ulaya

Ni kawaida kuona makocha wa jinsia ya kiume wakiwa wanafundisha timu za mpira wa miguu za wanawake, lakini ni mara chache sana tumewahi kushuhudia kocha wa kike akiwa anaifundisha timu ya wanaume.
Lakini klabu ya ligi daraja la kwanza ya Ufaransa Clermont imeweka historia mpya kwenye soka la nchi hiyo kwa kumtangaza mwanamama Helena Costa kuwa kocha wao mpya kuanzia msimu ujao, na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza kufundisha soka la hadhi ya juu nchini Ufaransa. 
Costa, 36, alikuwa kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya Irani tangu mwaka 2012 lakini sasa amekubali kumrithi Regis Brouard kwenye klabu ya Clermont.
Helena ambaye ni raia wa Ureno, aliwahi kufanya kazi kama kocha mkuu wa kituo cha soka cha klabu ya Benfica na timu kadhaa nyingine nchini Ureno, ambapo aliweza kushinda makombe kadhaa. Pia aliwahi kuifundisha timu ya wanawake  ya taifa ya Qatar.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad