Lowassa Alipigwa Marufuku Kuendesha Harambee, Sitta Anagawa Pikipiki na Baiskeli Anaangaliwa Tu

Mh. EL alipigwa stop na chama chake shughuli mbalimbali za kijamii ikiwamo ya kuendesha harambee kwa tafsiri kuwa, ni dalili za rushwa kwa ajili ya kusaka uraisi. Je mbunge wa Irambo, Waziri wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa BMK pamoja na mkewe kugawa pikipiki 16 na baiskeli 95 kwa viongozi wa chama chake ni nini?

Nayo ni kama ya Lowassa na wenzake tu. Kitu kimoja kinachonishangaza ni kuwa CCM iliona kuanzia lini kuwa ile ni rushwa. mbona wote wamefanya hayo hayo? Mbona wamekuwa wanagawa uji, pombe, unga na wali kwa miaka mingi tu? Mbona wana tabia ya kugawa nguo na hela ndogondogo? Au inakuwa siyo rushwa wakati wa uchaguzi ukifika, ila sasa ndiyo rushwa?

Mi nadhani waache unafiki tu. Kama jini umelinunua mwenyewe usilalamike likianza kula wanao! Vinginevyo my concern wananchi,ambao kila siku wanahongwa uji, wali na vichenji vichache, ili wauze kura zao. Unanunuliwa kwa sahani ya wali ya mlo mmoja,halafu unavumilia maumivu ya maisha duni kwa miaka 5!

Nadhani Watanzania ni watu wa ajabu sana! Nadhaninikiwa namalizia masters itabidi research iwe ni "mentality ya Tanzania"
Source:JF
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad