Maskini:Familia Yamwachia Mungu Kifo cha Meneja Ewura

Aliyekuwa Meneja wa Biashara ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Julius Gashaza anazikwa leo katika Kijiji cha Mulukulazo, Ngara mkoani Kagera huku familia yake ikisema haina cha kusema kuhusu kifo hicho, bali inamwachia Mungu.
Akizungumza jana kijijini hapo, mdogo wa marehemu, Alex Gashaza alisema familia imepokea msiba huo kwa mshtuko mkubwa na kushangazwa na taarifa kwamba ulitokana na kujinyonga kama inavyodaiwa.

Alisema baada ya kupokea simu kutoka Dar es Salaam kuhusu mazingira ya kifo hicho, wameshindwa kujua sababu za kifo kwa kuwa hakuna mtu aliyezungumza naye.

Alisema kaka yake hakuwa na tatizo lolote na wanafamilia, ndugu wala jamaa zake wa karibu, hivyo familia haiwezi kuelezea jambo ambalo halina ushahidi, badala yake inaacha tukio hilo mikononi mwa Mungu.

“Tumekuwa tukishirikiana naye kuendeleza familia yetu, kama unavyoona nyumba ilipokuwa imefikia hatua ya kuezekwa, kuna mchango wake mkubwa kifamilia,” alisema Alex.

Mwili wa Gashaza ulitarajiwa kuwasili Mulukulazo jana jioni na leo saa 4:00 asubuhi utapelekwa katika Kanisa la Anglikana katika kijiji hicho kwa ajili ya sala na saa 6:00 mchana utaagwa kabla ya mazishi yatakayofanyika nyumbani kwake.

Kiongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza mkoani Mwanza, Mchungaji Lazaro Manjelenga ambaye pia ni baba mkwe wa mdogo wa marehemu, alisema wana matumaini na Muumba kwa kile kilichotokea.

“Siri ya Mungu na mwanadamu wake hakuna wa kuijua, hivyo tusihukumu,” alisema na kuongeza kuwa mazishi yatafanyika kwa mujibu wa taratibu za Kanisa hilo.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mungu atalipa.. R.i.p bro

    ReplyDelete
  2. Hivi mtu akijinyonga hizikwa kidini? Kwa mnaojua baelezeeni jamani. Unless huyu bwana iwe kanyongwa kitu ambacho wote hatuna uhakika ila ukweli uliopo ni kajinyonga basi hata kama alitishiwa maisha kiasi gani kujinyonga sio njia sahihi ya kufanya kwa vile unamkosea Mungu. Tuache unafiki hapa na wote tuwe wakweli huyu jamaa kama kajinyonga ama kwa kuogopa jela au mtu basi anaenda motoni hakuna cha rest in peace wala nini. Na hapaswi kuzikwa kidini. Ni hayo tu.

    ReplyDelete
  3. ww una hakika gani km kweli kajinyonga?acha habari zako ww ndugu yako ikitokea kajinyonga utamzika vip?jibu unalo mwenyewe sina hakika km kajinyonga au kauwawa kisha katundikwa kwnye kitanzi ni ngumu kujua kifo kimetokea vipi usicomment kitu km hujui

    ReplyDelete
  4. Polisi Imethibitisha Pasipo Shaka Kuwa Kajiua, Sasa Mtu Anaejiua Hapaswi Kuzikwa Kikanisa Na Mhusika Huenda Motoni Moja Kwa Moja.Hvy Mdau Hapo 4.15 Yupo Sahihi

    ReplyDelete
  5. peleka kule 8:07PM unakua motoni wewe?umekujaa uwoga tu

    ReplyDelete
  6. Kwa marehemu muhubiri msihubiri kwake sio kitu mahubiri huwa ni faraja kwa wale nd. marafiki waliofika katika mazishi. Kufanya mazishi ya kidini haya msongezi peponi wala kumuweka mbali na peponi marehemu. wanaumia ni wale walio baki. ndio yanaotakiwa kupewa faraja ya kila aina iwe ni mchango wa rambirambi, kuwa karibu na nd wa marehemu, kusaidia kazi mbalimbali nk.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad