Master Jay:Maproducer Tunanyonywa Sana Hata Sisi Tunahitaji Kuendesha Magari Mazuri

Mtayarishaji mkongwe wa muziki Tanzania, Master J ameeleza sababu zinazopelekea watayarishaji wa muziki nchini kutofanikiwa kama wasanii wanaowatengenezea muziki kuwa hutokana na mgawanyo usio sawa wa kipato.

Master J aemeiambia Bongo5 kuwa hali hiyo humfanya mtayarishaji wa muziki kuona maisha ya msanii aliyefanya nae kazi yaboreka huku yeye akiendelea kusota.

“Unakubali pale mwanzoni lakini mwisho wa siku unakuja kugundua producer nimenyanyuliwa na mtu kama Diamond mpaka hapa sasa najulikana na sifa zote lakini huna gari, huna uwezo wa kuvaa nguo nzuri, huna hela ya kuishi sehemu nzuri, kwahiyo mwisho wa siku unakuwa mtu wa kuchekwa tu. Ndio hapo producer roho huanza kumuuma anaanza kugombana na msanii,” amesema Jay.

Amesema hali hii ilimfanya astaafu muziki kwa kuwa aliona malengo aliyokuwa nayo wakati akianza kazi hiyo hayatatimia.

“Ndio maana hata mimi nikastaafu, mimi mwisho wa siku nilikuwa nataka watoto wangu wasome kwenye shule fulani, waende kwenye university fulani, nikaona hicho kitu nikaona nikiendelea hivi sitaweza kufanikisha hayo kwa kupitia muziki. Ndio maana nikachukua hela yangu ile Mungu alinijalia kwenye muziki nikawekeza kwenye biashara nyingine, bahati nzuri namshukuru mwenyezi Mungu alinipa akili ya kufanya biashara.” Ameongeza.

Amesema sababu kubwa ya kuwepo kwa hali hiyo ni producers kutokuwa na umoja ambao ungewafanya wawe na msimamo unaofanana, bei inayofanana na utaratibu ambao ungewawezesha kunufaika na matumizi ya nyimbo wanazotayarisha.

Source: Bongo5

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. shaa kashakuzingua na ksismi chake sasa tulia.........

    ReplyDelete
  2. mwe nana we kiboko!!lkn ndo vzr mana hata kama kuna mtu alikuwa kanuna atajikuta kacheka akisoma koment zako

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad