Mbeya City FC Yakubali Kipigo cha Mbili Moja Huko Khartoum

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
TAARIFA kutoka mjini Khartoum nchini Sudani usiku huu ni kwamba wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya CECAFA Nile Basin Cup, Mbeya City fc chini ya kocha mkuu Juma Mwambusi wamefungwa mabao 2-1 na AFC Leopard ya Kenya katika mchezo uliopigwa kuanzia majira ya saa 2:00 kamili usiku mjini Khartoum.
Bao la Mbeya City fc limefungwa na kiungo mshambuliaji, Deus Kaseke.
Hata hivyo inaelezwa kuwa mchezo huo ulikuwa mzuri kwa timu zote, lakini AFC walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza.
Ushindi huo unawafanya AFC Leopard wakae kileleni mwa kundi B baada ya kufikisha pointi 6.
Endelea kufuatilia mtandao huu, utakupatia habari kamali hivi punde.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wamewafumua wazee wa tummoghele

    ReplyDelete
  2. hawa za kimataifa hawaziwezi, tuliwaona hata mapinduzi cup

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad