Kelele, kukunjana na kunyoosheana vidole jana mchana vilitawala nje ya ukumbi wa Bunge wakati wabunge wa CUF kutoka Zanzibar walipotaka ‘kumkanya’ Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy.
Sakata hilo la aina yake lililodumu kwa takriban dakika 15 lilitokea saa 7:05 mchana baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuahirisha kikao cha Bunge.
Wabunge hao Mussa Haji Kombo (Chakechake), Kombo Khamis Kombo (Magogoni) na Muhammad Ibrahim Sanya (Mji Mkongwe), walitaka ‘kumkanya’ Keissy kutokana na kile alichosema alipokuwa akichangia Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mwaka 2014/15 na kusema Zanzibar haichangii katika Muungano, hivyo haina haki ya kuhoji mambo ya upande wa pili.
Kauli hiyo licha ya kulalamikiwa na wabunge wote wa CUF kutoka Zanzibar kiasi cha kufikia hatua ya kusimama na kuomba mwongozo wa Spika, Keissy alizidi kuwashambulia na kusema kuwa majimbo ya Zanzibar watu wake wanaweza kukusanywa sehemu moja kwa kupigiwa filimbi tu.
“Nyie Zanzibar idadi yenu ya watu ni asilimia 2.8 ya watu wote wa Tanzania. Sasa mnataka kupata kila kitu sawa ili iweje! Mnataka ajira asilimia 21 na Watanganyika wakafanye kazi wapi?” alisema Keissy.
Baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho na wabunge kuanza kutoka nje, wabunge hao wa CUF walikwenda kumsubiri Keissy karibu na jengo la kantini.
Mbunge wa kwanza kumvaa Keissy alikuwa Khamis Kombo ambaye kabla ya kumfikia alizuiwa na Mbunge wa Mpanda Kaskazini (CCM), Moshi Selemani Kakoso.
Wakati Keissy akishangaa alitokea Haji Kombo ambaye naye alizuiwa na Mbunge wa Mikumi (CCM), Abdulsalaam Selemani Amer.
“Mimi sitaki kupigana bwana ninachokijua ni kwamba nilikuwa nikichangia mjadala wa bajeti na nilichokisema ni ukweli mtupu,” alisema Keissy huku akiwa amenyanyua mikono yake juu na kuondoka eneo hilo.
“Wewe (Keissy) sijui una nini wewe. Unapenda kutufuata fuata sana watu wa Zanzibar. Hivi una nini wewe? Hivi hujui kuwa Tanzania ni Muungano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar?” alisikika akisema Khamis Kombo.
Kwa upande wake, Sanya hata baada ya wenzake kutawanyika eneo hilo, aliendelea kumlaumu Keissy na kuwataka wabunge wa CCM kumuonya.
“Anapenda sana kutoa kauli mbaya dhidi ya Zanzibar. Jamani mkanyeni mwenzenu haiwezekani kila siku awe yeye tu anayetukashifu bungeni,” alisema Sanya huku akitulizwa na mbunge wa Kibiti (CCM), Abdul Jabiri Marombwa.
kunaukweli ndani yake kwani tunalingana idadi ya Zenji? kwanini haki iwe sawa?
ReplyDeleteKama haki si sawa katafteni nchi mnayolingana population den.muungane
ReplyDeleteWenyewe mlikubali kuungana kwa nn muwabague tens? Ndio maana wanzanzibar hawautaki muungano nyinyi mnawangangania tuu. Kama mnataka muungano wapewe haki sawa
ReplyDeleteHaki sawa itoke wapi wewe acha uchoko wazanzibari kwanza wanategemea kila kitu uku nyie mnajua kupika urojo tuu ndio maana mmeregea sanaa kila kitu mnataka bara wawafanyie
DeleteWapeww haki sawa ya nini na wenyewe kanchi kao kadogo, anavyowaaambia sawa sawa wamezidi wazanzibar kila siku waseme wao wakiambiwa ukweli wanakasirika sawa sawa alivyosema pumbavu zao kwanza hamna hata anayewang'ang'ania wampindue rais wao wakitenge, kwanza hamna hata mtu wa bara anayefaidila zanzibar PUMBAVUU ZAO
ReplyDeleteHuna sababu yakutukana,toa maoni yako tu bila matusi.
ReplyDeleteMbona wazanzibar wakisema hawataki muungano mnawang'ang'ania uvunjeni basi
ReplyDeleteNani anawangangania zaidi ya Muislam Mwenzao Kikwete ? waende zao Bwana kutwa kucha wao kulalalama tu kama wanawake wajawazito
ReplyDeletewapige kura ya kujitoa kwenye muungano,nini bara inapata kule?karafuu ya kuweka kwenye vishungi vya sigara?
ReplyDeleteMdini utamuona tu hata yasiohusu dini yeye ataweka udini, muasisi kutoka bara alikuwa islamu,
ReplyDeletenyinyi ccm msiwe wajinga inonyesha wengi wenu siasa hamjui mkifika hapo bungeni wengine hamjui hata kuchangia hoja,mimi nashauri wabunge wote wa ccm wapatiwe mafunzo ya muda mfupi kabla ya bunge kuanza kuliko kuropoka kama hivyo,vingnevyo wapewe nchi yao kwakufanya hivyo kutakua hakuna malalamiko. Mnawatawala halafu mnawajibu jeuri na kebehi ju,Je ni uungwana huo?
ReplyDeletembona ccm mnajikanyaga hamuwaambii ukweli wenzenu ccm zenji muungano si lazima kama mmeshindwa basi kila mtu akamate chake acheni kutafuna maneno msiwabughuzi wazenji.
ReplyDeleteMBUNGE KEISSY NI WA PILI KUTAMKA UKWELI HUU BUNGENI WA KWANZA ALIKUWA TUNDU LISSU...MUUNGANO UMEWAPA AJIRA NYINGI,MSIANGALIE TU MABALOZI, JIHESABUNI BUNGENI,JESHINI, POLISI,MADUKA BARA N.K. AU FURUSA HIZI ZA UPENDELEO HAMZITAKI MNATAKA UBALOZI TU?
ReplyDeleteMie nawashangaa sana hawa ndugu zetu wa Bara! kitu kidogo maduka yenu bara sasa mbana wahindi na waraabu wa Yemen wanamaduka kibao dar wamuwasemi seuze wanzanzibar! usituletee ubishoo kwani lazima Muungano!?
ReplyDeleteSasa kama Wazanzibar ni asilimia 2.4 % basi tuwacheni wenyewe tujitawale kwani ina ulazima gani kutung'ang'ania kama mpira wa kona kama hamna maslahi na sisi? ndio tuseme mnatuonea huruma sana hatuwezi kujitawala?
Sasa inatosha tena ni wakati wa wazanzibari kujikombona na mkoloni mweusi- ''Abeid Aman Karume alitwambia kuwa kama koti likiwabana basi mlivue sasa naona linatubana tena sanaaa'''
alichokiongea kesy ni kweli tupu hatuwezi kuwa pasu na znz ikiwa taganyika ina mikoa zaid ya 27 upungufu wa kufikiri
ReplyDeletelakinin kama hamfadiki na muungano mbona mnawangangania wazanzibar basi si waachieni nchi yao michogo nyi mikafiri mishenzi
ReplyDeleteIsikosoe uumbaji wa Mungu kwa kutuita machogo na wala Mungu tunaemwabudu ss hakutuambia kama kuna kiumbe chake kinachoitwa KAFIRI... poleni sana enyi waabudu shetani...
Delete