Mbwana Samatta Amtaja Aliyeimaliza Stars

Kwa wale waliotazama mchezo huo, Mahachi alikuwa amevaa jezi namba 11 na riboni mkononi ambapo alikuwa akiisumbua sana safu ya ulinzi mara kadhaa.

Akizungumza na Championi Jumatano, Samatta alisema Stars ilijitahidi kutokana na hadhi ya Zimbabwe kuwa kubwa kwani wameshiriki michuano ya Afcon mwaka jana, hata hivyo uelewano baina yao uliwasaidia sana kupata ushindi huo, japo ni kiduchu.

“Kuna jamaa sikumkariri vizuri na jezi yake, lakini alikuwa akitumia sana mguu wa kushoto, mwenye rangi nyeupe kichwani, kweli alitusumbua mara kadhaa, ingawa tunashukuru tumepata ushindi.
“Ilikuwa mechi ngumu, lakini nafikiri kwa kuwa tunaongea lugha moja (Kiswahili), ilichangia kuelewana zaidi na kucheza kwa umakini kutokana na wapinzani wetu kuonekana kubadilika baadaye na kutushambulia,” alisema nyota huyo.
GPL
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sasa msiende kumbwela uko zimbabwe maana hamkawii kuaribu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad