LIONEL Messi amekubali kusaini mkataba mpya katika klabu yake ya Barcelona na kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani ambapo atakuwa anavuta mkwanja wa paundi milioni 16.3 kwa mwaka.
Baba yake, Jorge, amekutana na maofisa wa klabu Javier Faus na Antoni Rossich wiki iliyopita na kusaini mkataba wake wa 7 ndani ya klabu ya Barcelona.
Messi ambaye mwezi juni atafikisha miaka 27 baada ya kuongeza mkataba huo, sasa atakaa Barcelona mpaka mwaka 2018.
Malipo atakayoyapata Messi kwa mwaka yamemfanya amuangushe nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo aliyekuwa anavuta paundi milioni 15 kwa mwaka mbali na marupurupu.
sasa unafikiri mesi ni team gani inamtaka? Ht mkimtoa bure
ReplyDeletembeya city inamtaka
DeleteAbajalo ya sinza leo kesho wanamtaka!
DeleteSafi sana messi. make sure leo unatupatia ubingwa wa laliga kwan uko njema.
ReplyDeletewewe atletico anachukua io ipo wazi, haina mjadala... Messi kiwango kwisha c messi yule wa enzi izo
ReplyDeletehahahaaa mdau, eti mbeya city inamtaka mesi...wkt ht tambwe amewashinda kumng'oa msimbazi
ReplyDelete