Mkurugenzi wa Tanesco wa Zamani na Mkewe Wapandishwa Kizimbani

MKURUGENZI  wa zamani wa Shirika la Umeme nchini, (Tanesco) William Geofrey Mhando na mamsap wake, Eva Stephem Mhando, na maofisa wengine watatu wa shirika hilo, France Lucas Mcharange, Sophia Athanas Misidai na Naftali Luhwano Kisinga,  leo wamepandishwa kizimbani Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam kwa kosa la kuhujumu uchumi na kuiingizia serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni 884,550,000.

Katika kesi hiyo iliyosomwa na Wakili wa Serikali, Leonard Swai, mbele ya Hakimu Frank Mushi, wakili huyo alisema Mhando akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco anatuhumiwa  kumpa tenda mamsap wake ya kusambaza vifaa vya stationery vyenye thamani ya shilingi milioni 884,550,000/ kwa shirika hilo kinyume na taratibu.

(PICHA : RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY/GPL)
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tanzania ingekua hivi basi ingekua tuko mbali kwa maendeleo!

    ReplyDelete
  2. siku mbili utasikia wako huru hawana hatia chezea tz na sheria

    ReplyDelete
  3. Kesho tu mnawaachia selikal kuwen na msimamo mfyuuuu

    ReplyDelete
  4. Swala ni kwamba kwenye kesi hizi serikali haina wanasheria mahiri. Halafu kumbuka waajiriwa wengi wa serikalini ni wale walio pata level za kawaida shuleni....with exception ya BoT. Idara nyingi utakuta ni hao wenye bora degree. Sasa wakienda mahakamani wanakutana na wale wanasheria waliokuwa vipanga shuleni unategemea nini? Na kumbuka mahakamani ni argument ndo zinasound...halafu weka na 'sabuni ya roho', hao wanasheria wa serikali wanalipwa pennies...na when you pay peanuts you get monkeys. So msililie mahakama tu...lilieni mfumo wa ajira na uwezo wa waajiriwa.
    Kumbuka kesi zinaanzia polisi kuchunguza...polisi wetu majority ni form 4 form 6 failures...ndo wanakuwa wapelelezi...wanapeleleza wizi wa mtu ambaye ni professor au masters holder...Ongeza na zako

    ReplyDelete
  5. Swala ni kwamba kwenye kesi hizi serikali haina wanasheria mahiri. Halafu kumbuka waajiriwa wengi wa serikalini ni wale walio pata level za kawaida shuleni....with exception ya BoT. Idara nyingi utakuta ni hao wenye bora degree. Sasa wakienda mahakamani wanakutana na wale wanasheria waliokuwa vipanga shuleni unategemea nini? Na kumbuka mahakamani ni argument ndo zinasound...halafu weka na 'sabuni ya roho', hao wanasheria wa serikali wanalipwa pennies...na when you pay peanuts you get monkeys. So msililie mahakama tu...lilieni mfumo wa ajira na uwezo wa waajiriwa.
    Kumbuka kesi zinaanzia polisi kuchunguza...polisi wetu majority ni form 4 form 6 failures...ndo wanakuwa wapelelezi...wanapeleleza wizi wa mtu ambaye ni professor au masters holder...Ongeza na zako

    ReplyDelete
  6. rushwa inaanzia polisi mpk mahakamani, majanga

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad