"HAIWEZEKANI BADO TUNAMUHITAJI DIDIER KAVUMBAGU YANGA" CHARLES MKWASA

KOCHA Msaidizi wa Yanga Charles Mkwasa amesema aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo Didier Kavumbagu amefanya haraka kusaini Azam kwani alipaswa kusubiri hadi uongozi wa klabu hiyo kumpa nafasi hiyo.

Kavumbagu ambaye mkataba wake uliisha msimu uliopita, alisaini mkataba wa mwaka mmoja na Azam juzi kwa ajili ya kuwatumikia mabingwa hao msimu ujao.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkwasa alisema Kavumbagu bado mchezaji mzuri anayemwamini, ndio maana walikuwa wakimtumia katika mechi nyingi msimu uliopita na bado walikuwa wakimhitaji.

“Ni mchezaji mzuri, alikuwa akifanya vizuri na bado tulikuwa tunamhitaji ndio maana tuliweza kumtumia msimu mzima wa Ligi Kuu Tanzania Bara, amefanya haraka mno,”alisema.

Mkwasa alisema walihitaji kuwa naye lakini kama mwenyewe ameshindwa kuvuta subira na kukimbilia Azam, basi, hawawezi kumlazimisha.

Alisema kwa utaratibu wa Yanga huwa mchezaji anapomaliza mkataba wake, humwita na kuzungumza kumpa mwingine, hivyo, kama angeendelea kusubiri angeitwa na kuongezewa mkataba mwingine.

Kavumbagu alimaliza msimu wa Ligi Kuu akiwa amepachika mabao 13, nyuma ya Mrundi mwenzake anayecheza Simba Amis Tambwe aliyeibuka mfungaji bora kwa kupachika mabao 19.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ngoja ngoja huumiza matumbo!
    Mlitaka asubiri mpaka msimu wa usajili uishe ndipo mtangaze kumuwacha, akose muelekeo kama ilivyotokea kwa Kaseja. Hureeeeeee AZAM, biashara asubuhi!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Nashangaa sana mlikua mkisema Yanga wanasajiri majina lakini Leo hii mnashinda kwenye mageti ya Yanga kuchukua wachazaji walewale.

    ReplyDelete
  3. Azam wamechemka! Usajili wa wachezaji wa kigeni mwisho watatu Tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad