Mrema Aiombea heri Ndoa ya Chadema, CUF, NCCR

MBUNGE wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP ) ametaja ushirikiano wa vyama vitatu vinavyounda kambi rasmi ya upinzani bungeni kwamba ni ndoa ambayo kama wahusika wangekuwa na nia njema, ungeanza siku nyingi tangu Chadema kilipounda baraza lake mwaka 2010.

Mwanasiasa huyo ambaye ameunga mkono kauli ya Spika Anne Makinda, kwamba kambi hiyo rasmi ya upinzani imekumbuka shuka kunakucha, amekiri kwamba haelekei na wala hapatani na wana Ukawa; lakini yeye ni mpinzani na mzalendo wa kweli nchini.

Mrema alisema hayo juzi mjini hapa akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Alimjibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe ambaye katika kutangaza Baraza Kivuli la Mawaziri juzi, alisema mbunge huyo hana dhamira ya kuwa mshirika wa Ukawa na alishaweka wazi kuwa mshirika wa CCM.

Alitaja ushirikiano huo wa Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi, kuwa ni ‘ndoa’ anayoiombea kila la heri na hawezi kuibashiria mabaya, isipokuwa anachoona ni kwamba kama wangekuwa na nia njema, ndoa hiyo ingeanza siku nyingi tangu Chadema ilipounda baraza mwaka 2010.

“Ushirikiano huu ni jambo lao, wanafikiri litawasaidia. Lakini kwani hatujui walivyokuwa (CUF na Chadema) wakitukanana? Siwezi kuwabashiria mabaya. Wangelikuwa wema, hiyo ndoa ingeanza siku nyingi,” alisema Mrema.

Alisema yeye ni mpinzani ambaye kamwe hawezi kushiriki katika mambo ya kubomoa nchi.

“Kwanza mimi sijaomba huo uwaziri kivuli. Hawa watu ni wa ajabu sana... Mbona Maalim Seif (Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF), yuko kwenye Serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar. Mbona CUF hawaambiwi ni CCM? “Kwanza ukinilinganisha na wao, naona wananionea wivu. Nimeshika madaraka ambayo hawajawahi kuyashika. Mbowe hana sifa za kuniteua. Ana sifa ipi sasa?.”

Mrema alitamba kuhusu nafasi za uongozi serikalini alizowahi kushika, ikiwemo ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana na Naibu Waziri Mkuu.

Alisema licha ya kuwa miongoni mwa watumishi waliotukuka, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 akiwa NCCR Mageuzi, alipata kura milioni 1.8 ambazo kwa mujibu wake, hakuna mpinzani anayeweza kuzipata.

“Na nilikuwa NCCR Mageuzi. Si watu wangenikataa kuwa mimi ni CCM…Nani amewahi kuvunja rekodi hii ya kura?” Alihoji.

Akiendelea kutamba kwamba hatishiwi na cheo chochote, alisema aliamua kuachana na kile alichoita ‘biashara ya jumla’ akimaanisha kugombea urais na badala yake, akaingia kwenye ‘biashara ya reja reja’ kwa maana ya ubunge.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe Mrema ,kama wapinzani wamechelewa kufunga ndoa na sasa unawatakia kheri kinafiki,tuambie je wewe mrema uliyefunga ndoa ya mkeka na ccm miaka mingi,wamekupachika mimba ngapi? Huna lolote,wewe ni 'msakatonge'tu.

    ReplyDelete
  2. Safi sana Mrema.ulichoongea ni ukweli mtupu! Ukawa wataishia kunawa,wapuuzi wakubwa hao!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ungekuwa na akili ungewashukuru wabunge wa upinzani kwa kuibua madudu na ufisadi ambao paka wa bar kama wewe kamwe usinge weza kuujua!watanzinia wengine bwana hawana uchungu kabisa na nchi yao pamoja na madudu wizi wa hawa viongozi walafi leo kuma kama hawa wanauponda upinzani!utabaki kuwa masikini kenge wewe.

      Delete
  3. hawa cdm wasenge sana cuf walipounda umoja wa kitaifa walisema cuf sio wapinzani tena sasa imekuwaje,hapa lazima tukubali cdm wanatapata namna ya kuokoa jahaz linanalizama baada ya kumzingua jembe letu zito

    ReplyDelete
  4. Kuna huyu anonymous anayeandika sana kumsifia zitto eti ni jembe.Kweli zitto ni jembe lakini la kumchimbia kaburi yeye na vyama vya upinzani.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio anajichimbia yeye na ccm?

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad