Mtoto Afichwa Kwenye boksi Miaka Minne

Mwanamke aliyetambuliwa kuwa ni Mariamu Said mkazi wa Kiwanja cha Ndege, Morogoro juzi alishushiwa kipigo na wananchi kutokana na kumficha mtoto wa marehemu mdogo wake kwenye boksi kwa miaka minne.
Tukio hilo lilitokea juzi saa nne asubuhi baada ya majirani zake kutoa taarifa kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Dia Zongo kuhusu mtoto huyo, Nasra Rashid, kufichwa ndani ya boksi tangu akiwa na umri wa miezi tisa.

Zongo alisema majirani hao walimweleza pia kuwa jirani yao huyo hamfanyii usafi mtoto huyo wala kumtoa nje.

Baada ya kupata taarifa hizo, Zongo alimtafuta Mwenyekiti wa Mtaa huo, Tatu Mgagala na kuongozana naye hadi kwenye nyumba hiyo na kumhoji mwanamke huyo ambaye alikuwa akijibu kwa kubabaika.

Moja ya maswali aliyoulizwa ni idadi ya watoto wake na akajibu kuwa ana wawili lakini wakati akiendelea kujibu maswali, ghafla mtoto huyo alipiga chafya na kuanza kukohoa, hivyo kuwapa wasiwasi na kuamua kuingia chumbani kwa mwanamke huyo kwa nguvu na kumkuta mtoto Nasra akiwa ndani ya boksi.

Ofisa mtendaji huyo alisema wakati wakimtoa mtoto huyo ndani ya nyumba, kundi kubwa la watu waliokuwa na fimbo na mawe walianza kumshambulia mwanamke huyo na kumlazimu mtendaji kutoa taarifa polisi.

Alisema muda mfupi baadaye, polisi waliwasili na kumkamata Mariam na kumpeleka katika ofisi ya kata ambako aliwekwa chini ya ulinzi.

Baadaye aliwekwa rumande katika Kituo Kikuu cha Polisi, Morogoro na mtoto alipelekwa Ofisi za Ustawi wa Jamii.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alisema wanaendelea kukusanya taarifa za tukio hilo ikiwamo matokeo ya vipimo vya madaktari kuhusu afya ya mtoto huyo kabla ya kuchukua hatua zaidi.

Kamanda Paulo alisema watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa kosa la kumfanyiwa mtoto vitendo vya kikatili.

Hata hivyo, kamanda huyo alisema polisi wanakadiria kwamba mtoto huyo alianza kufichwa kwenye boksi hilo akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu.

Utetezi wa Mariam

Akijibu maswali ya polisi, mwanamke huyo alikiri kuanza kumlea mtoto huyo tangu akiwa na umri wa miezi tisa baada ya mama wa mtoto huyo kufariki dunia mwaka 2010.

Pia mtuhumiwa alikiri kwamba mtoto huyo hajawahi kupewa chanjo yoyote wala kupelekwa kliniki.

Alikuwa akitoa maelezo hayo huku akiwa amemshikilia mtoto huyo aliyetapakaa uchafu ikiwamo haja kubwa na ndogo alizokuwa akitoa ndani ya boksi na kusema kwamba mara ya mwisho alimwogesha Julai mwaka jana.

Pia alisema alikuwa akimwekea chakula na maji ndani ya boksi lililokuwa nyuma ya mlango wa chumba.

Mume wa mwanamke huyo, Mtonga Ramadhani anayefanya biashara katika Soko la Mawenzi, Morogoro ambaye pia anashikiliwa na polisi, alidai kuwa hakuona sababu ya kutoa taarifa za kufichwa kwa mtoto huyo kwa sababu hamhusu na wajibu wake ni kutafuta chakula.

Alivyonaswa

Baadhi ya majirani wa mwanamke huyo ambao hawakutaka kutajwa majina, walisema Mariam alihamia katika nyumba hiyo mwaka 2010 na hawajawahi kumwona mtoto huyo akitolewa nje wala kufanyiwa usafi.

Walisema mtoto huyo alibainika baada ya kusikika akikohoa na kulia nyakati za usiku, jambo lililozua wasiwasi kuwa huenda mtuhumiwa alikuwa mshirikina anayefuga misukule.

Baba wa mtoto

Baba mzazi wa mtoto huyo, Rashid Mvungi alisema hakujua kama mwanaye alikuwa analelewa katika mazingira hatarishi.

Akihojiwa na Ofisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungamtitu, Mvungi alisema alimzaa mtoto huyo nje ya ndoa na amekuwa akituma fedha za matumizi kwa mama yake mkubwa.

Mvungi ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, alisema baada ya mzazi mwenzake kufariki dunia alishindwa kumchukua mtoto wake kwa sababu tayari alishakuwa na mke.

Post a Comment

26 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Binaadamu mmh unawezaje kufanya hivo Mungu atusaidie

    ReplyDelete
  2. huyo mama alichofanya na mumewe sio utu kabisa hata sijui lengo lao ilikua nini mpaka mtese. mtoto wa mwenzen hivyo. haya mtavuna mlichopanda

    ReplyDelete
  3. Mtendaji alitakiwa awaache wananchi wawafundishe adabu pumbavu zao hao sio watu kabisa

    ReplyDelete
  4. freemason hao

    ReplyDelete
  5. Wanaume hawa mungu awape roho ya kuthamini damu zao..mtoto wako miaka 4 hutamani hata kumwona kisa kuzaa nje ya ndoa..mtoto kakukosea nini hata mzazi mwenzio kaburini kajisikia vibaya..huyo dada na mumewe ni vichaa kma huwezi kulea mtoto wa nduguyo acha wanaoweza watamlea...wamemtesa mtoto sana ila mungu yupo..

    ReplyDelete
  6. jamani sina lakusema zaidi nimeumia kupita kiasi lakin mungu yupo na atamlinda na atakuwa na maisha ya furaha baada ya mateso hayo. weeee mama uliefanya hivyo mungu atajua cha kukulipa sisi tunamuachia yeye muumba vyote.

    ReplyDelete
  7. Inasikitisha sana bidamu kukosa utu kiasi hicho,namwomba huyo mtoto nimtunze jamani,huyo mama ni muuaji na alipie dhambi zake.

    ReplyDelete
  8. Huyo mama pamoja na mme wake niwashirikina! Hao wote wawili ni wanga, mafanikio yao ni huyo mtoto. Sheria ifuate mkondo kwa wote wawili.

    ReplyDelete
  9. YAN BINADAMU TUMEKUWA WANYAMA KWELI HATA ROHO YA HURUMA HATUNA!MI NNGEMPGA NA HATA HUYO MUME WAKE MANA NAE ANA ROHO YA MKEWE HATA KUMUHURUMIA MTT,NA HATA BABA MZAZ WA MTT ANA ROHO MBAYA UMEZAA NJE SAWA,UNATUMA PESA ZA MATUMIZI SAWA KWAN MTT ANATAKA PESA MTT ANAHITAJI UPENDO HAPO MTT WA WATU ALIKUA SAWA NA YATIMA JAMAN....FUCK YOA ALL INHUMANS BOKO HARAM MTAENDANA NAO SAWA

    ReplyDelete
  10. Waliomtesa huyo motto ni wauaji na wapewe adhabu kali sana maana hata huyo motto angekufa hakuna mtu angejua na wangeweza pia kuzika kimya kimya, ila baba mzazi wa motto nayeye achukuliwe hatua kwa uzembe. Haiwezekani uzae motto tena unajua anapoishi then ipite miaka minnee I mean 4 solid years hujaenda kumuona motto wako kisa umeoa, kwani si uliona baada ya mama wa motto kufariki, what so special ushindwe kwenda kumsalimia mwanao damu yako mwenyewe kweli wanaume mnachangia kwa kiasi kikubwa mateso wanayopata watoto. Ina maana huyo baba wa mzazi hakumtaka huyo mtotoo na aliona ni kama mzigo umemuondoka and am not sure kama kweli aliwahi kutoa hela za matumizi and if it is yes basi na yeye ameshiriki kwenye huo unyama direct or indirect.

    Naomba adhabu kali itolewe kwa wote watatu, wana element za uuaji. Halafu baba mzazi ni eti MTUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOROGORO kweli mji huo huo aliopo motto wako unakosa even ten minutes za kwenda kumuona, hata ungewaomba walezi wakuletee angalao mahali uione tu sura ya binti yako wewe baba ni muuaji kabisa. Nilifikiri uko hata nje ya mkoa wa kumbe uko mkoa mmoja na binti anateseka anaishi kama msukule since last year hajaoga mateso gani hayo jamani, na huyo mwanamke mwenzetu pamoja na roho mbaya bado ni mchafu hivi harufu ya mavi na mikojo ya motto unawezaje kukaa nayo ndani kwa more that two days???? mbona nahisi ushirikina hapo.

    ReplyDelete
  11. Huyu mtoto nilipomuona kwenye TV nililia ni kwamba hata hiyo mikono imepinda yaani amelemaa halafu kanajibu kila anachoulizwa jamani Mungu atusamehe binadamu wana roho mbaya saaana, wanaume tulieni basi michepuko sio mizuri mbona shimo ni lile lile? kama ni kibamia vaa soksi tatu basi ili itoshe kuliko kuchepuka, yaani siingilii mahakama lakini mimi ningeanza kunyonga baba wa mtoto halafu walezi wanafuata. katika maisha sipendi mtu yoyote anayetesa watoto hata wa wakaribu yangu wanajua hilo.

    ReplyDelete
  12. binadamu wamebadilika sanaaaaaa hivi unawezaje kumuweka mtoto ndani ya box miaka minne, dhambi yako haifutiki hata uombe msamaha shwain wewe, na hii itakutesa vizazi vinne, ujue binadam hawajui kuwa wakitenda dhambi itakuja kumtesa mwenyewe badae, na kama si mwenyewe lkn vizazi vyake, vitukuu na vilembwe, mpaka vizazi vinne si mchezo, utakuwa unateseka unaanza kusema mungu nimekukosea nini kasahau kabisa kuwa yeye alimtesa mtoto wa mwenzie miaka mingi iliyopita, malipo ni hapa hapa duniani akhera hesabu asubirie tu na yeye atakuwa keshasahau atazunguka kwa waganga wa kila aina hapati tiba atsingizia mara karogwa na jirani, mara bibi yake, anasingizia watu tu kumbe kasahau kabisa alishatenda hili kosa.

    ReplyDelete
  13. halafu ati mtoto Mungu akimjaalia akakua akapata maisha mazuri msenge mmoja analalamika "mtoto hanijali" maana niliposema kwa Diamond nikaonekana mbaya leo yaoneni wenyewe, wanaume walivyo na roho mbaya, wanajua kutundika tu hawajui kulea mbwa hawa hata huko majumbani 80% ya watoto katika ndoa wanahudumiwa na wazazi wa kike, jamaa likirudi lishachovya lilipotoka linanuka shombo za kila aina, ati anasema alikuwa anatoa pesa ya matumizi, si kweli jamani mpare atoe pesa asijue inakwenda wapi huyu atakuwa si mpare kasingiziwa.

    ReplyDelete
  14. God hv mercy upon us....kitendo cha kikatili sana...dunia inaelekea kubaya....Bwana Mungu tumuombe sana.....4years in then box!ts better angemua ijulikane bt God z good ndo maana mtt kapata msaada.

    ReplyDelete
  15. Uyyo baba mzazi mchawi, na hao wanaomlea pia wachaw, mung amewaumbua kwa unyama walioufanya, ningekuwepo uyo mama angejuta kuzaliwa mwanamke, mamae zake

    ReplyDelete
  16. Hao wahukumiwe kifungo cha maisha!

    ReplyDelete
  17. Yani hao ni wachawi

    ReplyDelete
  18. Wanyongwe tu hawa watuuu, ni wauwaji kabisaaa. .rohoo mbayaa! !!!

    ReplyDelete
  19. Baba mzazi ndio mchawi. Miaka 4unatoa pesa bila kutaka kumwona mwanao? Anajua nini kilikuwa kinaendekea. Akibamwa atasema. Huyo hata mama wa mtoto alimuua yeye.

    ReplyDelete
  20. Huyo baba mzazi naye ni mnafki na yeye ahusishwe tu kwenye hiyo kesi moja kwa moja. Alikuwa hajui kivipi ina maana yeye alikuwa anatoa hela bila ya kumuona huyo mtoto kwa miaka yote hiyo 4?

    ReplyDelete
  21. Jamani huu ni ukatili wa hali ya juu,Lazima kuna jambo lillofichika hapo....Ama ushirikina au utahaahira tu.Na wasomaji wanoshambulia wanaume kuwa ni chanzo cha matatizo hawako sahihi.Imeelezwa kuwa amefanyiwa hivi na mama yake mkubwa.Labda niulize swali na hawa watoto wachanga wanaonyongwa na kutupwa mitaani mara kwa mara wanafanyiwa hivyo na wanaume???Tusinyoosheane vidole tuache unafiki kila upande una makosa yake.

    ReplyDelete
  22. wauwaji tuu ,wachawi haoo.wanyongwe

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad