Mwalala "Kuzidiwa Ujanja Yanga Aibu Sana"

BEN Mwalala ametoa la moyoni na kutamka Mrundi Didier Kavumbagu na Frank Domayo hawakukosea kusaini Azam FC, lakini kinachomsikitisha ni kitendo cha Yanga kuzidiwa ujanja.

Mwalala mchezaji wa zamani wa Yanga na mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara 2008 amekiri kuwa yeye ni mpenzi wa klabu hiyo na anaongea ikiwa inamuuma moyoni.

Ameliambia Mwanaspoti kuwa:”Hata Ulaya katika klabu kubwa, wanapoona mchezaji ambaye wanamhitaji, tena ni kijana wanamsainisha mapema hata kama mkataba wake haujaisha kabisa. Anaweza kuwa amebakiwa na miezi mitatu au zaidi wao wanamwongeza ndiyo Yanga inatakiwa kuwa hivyo.”

“Unapomuongezea makataba ni faida kwa timu pia, kwani hata kama timu nyingine itakapokuwa inamuhitaji lazima mumuuze kwa pesa nyingi,”alisisitiza Mwalala ambaye ni Mkenya.

“Hiki ninachokiongea kinaniuma, ninaongelea Yanga na mimi ni Mwanayanga pia, inabidi tujipange, bila kuwa makini yanaweza kuibuka mengine mapya.

“Kwa ukubwa wa klabu ya Yanga, ndiyo inayotakiwa kuiba wachezaji, lakini siyo yenyewe iibiwe kama tukio hili lililotokea,”alisisitiza.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukubwa pesa Mwalala, sio timu! Azam wapo vizuri 'kifedhwa" kuliko hao Yanga, ndo'mana wanaitwa MATAJIRI WA JIJI LA DAR

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad