Mwanasheria Mkuu Jaji Fredrick Werema Alikoroga..Atoa Kauli ya Kuudhi Bungeni

Kwa maneno ya siku hizi ni kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema ‘amelikoroga na kulinywa mwenyewe’, baada ya jana kutoa kauli ya kuudhi alipomtaka mbunge kutoka Zanzibar akaulize swali lake visiwani humo, iliyosababisha baadhi ya wabunge kususia Bunge na kutoka.

Kauli iliyoonyesha kuwagawa wabunge katika mafungu mawili; wa bara na Zanzibar, ilimlazimu Jaji Werema baadaye kusimama bungeni na kuwaangukia akiwaomba radhi waliokerwa na kauli yake na pia kuliomba radhi Bunge, Spika wake, Anne Makinda na wananchi.

Kuondoka kwa wabunge hao kulitokana na mwongozo wa Spika ulioombwa na Mbunge wa Ole (CUF), Rajabu Mbarouk Mohamed kutokana na majibu Jaji Werema kwa mbunge wa Mkanyageni (CUF), Habibu Mnyaa aliyekuwa ameomba ufafanuzi wakati Bunge lilipokaa kama kamati ya kupitisha vifungu vya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2014/15.

Mnyaa alisema Wizara ya Katiba na Sheria ni muhimu lakini imekuwa ndiyo ya kwanza kuvunja sheria na haki za binadamu na akataka ufafanuzi.

Hata hivyo, aliposimama kujibu swali hilo, Jaji Werema alimwambia Mnyaa kuwa mambo mengine akaulize Zanzibar na siyo katika Bunge la Jamhuri kwa kuwa si kila kitu kitaulizwa ndani ya Bunge hilo.

“Alichokizungumza Mnyaa ni sahihi lakini hapa si mahali pake, namshauri kuwa akaulize huko Zanzibar kwenye vikao vyao hapa sisi hatuna majibu,” alisema Werema.

Mara baada ya Bunge kurejea, Mbarouk aliomba mwongozo wa Spika akitaka ufafanuzi wa kauli hiyo kwamba ilikuwa ya kibaguzi.

“Mheshimiwa Spika, huu ni ubaguzi na haupaswi kufanywa na mtu msomi kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali,” alisema Mbarouk.

Alisema ubaguzi huo umewabagua wabunge ambao wamekula kiapo cha kulitumikia Bunge la Jamhuri ya Muungano na unaonyesha namna ambavyo Wazanzibari wanabaguliwa.

“Mheshimiwa Spika, yanapofanyika mambo kama hayo na wewe mwenyewe uko hapa unaona ni sawa na kubariki jambo hilo, huu ni ubaguzi unaoufanya wewe kwa kuwa lilifanyika ukiona bila hata ya kukemea,” alisema Mbarouk.

Hata hivyo, Spika alipinga na kusema: “Hakuna mwongozo wowote kwa kuwa hata wewe umevunja sheria kwani hata nilipokuambia kaa chini umeendelea kuzungumza, tunaendelea.... Katibu (akimtaka Katibu wa Bunge kutoa mwelekeo wa shughuli iliyokuwa inafuata ambayo ilikuwa Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).”

Baada ya kauli ya Spika, wabunge wa Zanzibar walihamasishana na kuamua kutoka nje kwa wakati mmoja na huku wenzao wa upinzani wakiendelea kutafakari cha kufanya. Wakati huo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe alikuwa akisoma hotuba yake.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu Werema kila akifungua mdomo wake utadhani ni mtoto mdogo kaamka tu usingizini hajapata fahamu nzuri.Ni mropokaji anayejaribu kumuiga binamu ya Wassira lakini hana narudia hans hekima wala busara kabisa.Aibu.

    ReplyDelete
  2. Jaji Werema una sura mbaya,akili mbaya,hulka mbaya,ulevi mbaya,tabia mbaya,taswira mbaya,ubaguzi mbaya,ulafi mbaya,historia mbaya na roho mbaya!!!!!

    ReplyDelete
  3. mura Werema ulichowaambia hao wazenji ni sahihi wao wana baraza lao la wawakilishi wakaulize huko, sie wabara hata kuingia kwenye baraza lao hatuingii je huo si ubaguzi ila hausemwi, sie watanganyika sijui tumerogwa na nani tunavyo wanyenyekea wazanzibari, kama kutoka bungeni waache watoke tu tuone kama shughuli za bunge hazitaendelea. Hata huo msamaha hukutakiwa kuwaomba hao labda ni shinikizo ulilopata kutokana na wadhifa wako tu. aah wazenji tumewachoka bwana Big up Mura Werema ni muda wa kuwapa makavu hao wazenji..

    ReplyDelete
  4. HIZO NDO CHANGAMOTO ZA MUUNGANO,TUNAPOSEMA ZANZIBAR NI KOLONI LA TANGANYIKA HATUELEWEKI HAYO NDO MATOKEO YAKE.KAMA HUYO MBUNGE ANAPASWA KUULIZA SWALI HUKO KWAO ZANZIBAR ILIKUAJE MKAKUBALI AINGIE KWENYE BUNGE LA TANGANYIKA?CCM ACHENI UONEVU NA KUWABURUZA WATU

    ReplyDelete
  5. Kama huyo mbunge hakutakiwa kuuliza swali kwa nini asimame na kama Werema yuko sawa kwa nini aombe msamaa? Acheni hizo kama vipi Bunge la Jamuhuri libaki la CCM na wapinzani wawe Zanzibar kwa sababu huku Bara hawana sauti UKAWA pambaneni sana wazee mtutoe kwenye majanga haya leo Liziwan hafanani na Makongoro

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad