Ndoa ya Mil 96 ya Vicky Kamata Hati Hati Kufungwa, Mizengwe Yaanza

ILE ndoa inayodaiwa ikifungwa harusi yake itatafuna shilingi milioni 96 kati ya Mbunge wa Viti Maalum Geita kwa tiketi ya CCM, Vicky Paschal Kamata na mwanaume aliyejulikana kwa jina la Charles iko katika hatihati ya kufungwa kutokana na kuibuka kwa mizengwe.

Habari za ndani zinadai kuwa mizengwe iliyoibuka katika hatua za mwisho zimemfanya mwanaume huyo kuamua kubatilisha ndoa ambayo ilikuwa ifungwe Mei 24, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

“Kuna mizengwe mingi sana kwenye hii ndoa japokuwa iko katika hatua za mwisho lakini hatihati. Wapo watu wanasema kuwa mwanaume  anadaiwa ana mwanamke mwingine, wengine wanasema ana mchumba ameshamlipia mahari kwa wazazi wake kwa hiyo mambo yameshajulikana na jamaa akaona aachane na ndoa hiyo.

“Lakini katika yote hayo, ukweli ni kwamba kuna asilimia tisini ya ndoa kutofungwa hiyo Mei 24 ndicho ninachokijua mimi,” alisema mtu mmoja wa karibu na familia ya wachumba hao.

Vicky alipotafutwa kwa njia ya simu Jumamosi iliyopita iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Hata hivyo, Uwazi bado linayafanyia kazi madai hayo ambayo ni mazito na ya ndani.

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mchumba sio mke ni rafiki anayetarajia kuwa mke/mme,Kutoa mahali sio kuoa ni kufuata taratibu wa kuoa.Hizi sio sababu labda kuna mengine.Watu wanasemehe hata mahali, nyumba, mashamba, familia nn ww?Kamata Vicky Kamata.

    ReplyDelete
  2. mh waoane tu km wanapendana kweli ilakm mmojawapo msanii bora ndoa ivunjwe

    ReplyDelete
  3. Mwanaume anamaisha yake na mkewe vick ana force hata mahari kajilipia mwenyewe aibu sana

    ReplyDelete
  4. Hizo milioni 96 mnazofuja mngetumia hata kujenga shule vijijini. mnaoana kwa mbwembwe halaf baada ya mwezi mnaachana.

    ReplyDelete
  5. Dume amestuka shamba lililimwa kwa majembe ya mkono plau na matrekta lazima alale mbele

    ReplyDelete
  6. iv me nilijua anaolewa mume aliezaa nae watoto, kumbe sio... Duh

    ReplyDelete
  7. Kama hayo yanayosemekana ni kweli basi hiyo ndoa haitadumu hata kidogo...Hayo mambo sio ya kucheza nayo na asimchezee Mungu.Naamini Mungu atampa nguvu mke wa huyo kaka ..Yetu macho tuone hiyo ndoa

    ReplyDelete
  8. chakula ya mheshimiwa hii, hapatakuwa na ndoa hapo!

    ReplyDelete
  9. mmmmh bosi wa ......... atakubali?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad