Ndoto "mpya" ya kakobe yaitesa ukawa!

 Kama ilivyo kawaida kwa askofu Kakobe kuota ndoto mbalimbali kuhusu mambo yanayohusu mstakabali wa taifa letu. Askofu Kakobe ameota ndoto nyingine ambayo inawahusu UKAWA na harakati zao za kudai katiba ya wananchi.

Katika ndoto hiyo ya askofu Kakobe ambayo ameitoa leo katika ibada ya jumapili kwenye kanisa lake, amesema kuwa, kutokana na hali ya ubaguzi uliokithiri kwenye upinzani kupitia umoja wao huo wa UKAWA, haoni kama kutakuwa na mafanikio yoyote ya malengo ya wana UKAWA.

Askofu Kakobe katika kufafanua alieleza kwamba, viongozi wa UKAWA hasa mhe Mbowe hakuwa sahihi katika maamuzi yake ya kuwatenga waasisi wa upinzani nchini, akimaanisha mhe Mrema. Hivyo, kitendo hicho cha ubaguzi kitaondoa baraka iliyokuwa imepandikizwa awali kwenye umoja huo.

My take,

Ni vyema sasa mhe Mbowe akachukua onyo hili na kufanya maamuzi sahihi ya kumuunganisha mhe Mrema na UKAWA. Kwa kuwa wote tunajua nguvu ya kiutabiri aliyonayo nabii Kakobe.
Tags

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mrema alikataa mwenye kuungana na ukawa, labda kakobe hasomi magazeti..na lini mrema amekuwa against serikali..maana yeye ndiye amekuwa hata akiua kila.chama anachokuwa..Siiuoni umuhimu wa Mrema ukawa..

    ReplyDelete
    Replies
    1. True 100%

      Delete
    2. Umepatiaaa Mrema kbaraka

      Delete
    3. Huyu mrema ni kibaraka mbaya sana na ukawa wangemuingiza basi wangekuwa wameharibu kila kitu!anatumiwa na ccm kuua upinzani huyu mwenye sura kama goti la nyani.

      Delete
  2. Kakobe, alisema Mrema ni Chaguo la MUNGU, inamaana MUNGU wa Kakobe anasemaga Uongo?

    Mungu wangu haongopi maana sio binadamu, Mungu ninayemuamini akisema ndiyo ni ndiyo na siyo siyo

    Siasa, ni vema zikaachiwa wanasiasa na Dini ziachiwe wana dini, vinginevyo tunakuwa tunamlazimisha MUNGU eti "Mrema ni Chaguo lake" wakati ni chaguo la wana Vunjo

    ReplyDelete
  3. Kakobe anaweweseka baada ya nguvu za giza alizokuwa anazitumia kukusanya watu kwisha muda wake na sasa walokole wake wengi wamemkimbia.Hata hivyo asimtaje taje Mungu kwani ni tapeli aliyekusanya kishirikina mabilioni ya shilingi,viroba vya gold na kuvunja ndoa za watu.Kama anataka kufanya siasa ni bora apande jukwaani akapambane huko.

    ReplyDelete
  4. Nyie binadam achen kuhukumu maana haki na hukumu zatoka kwake yeye muumba wa mbingu na nchi, usimnyoshee mtumishi wa Mungu kidole maana kinaweza kukuralua

    ReplyDelete
  5. kakobe acha ushirikina kwanini w.wke wote wanaosali kanisani kwako unawalazimisha wafunge vilemba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kakobe ni mtumishi wa Mungu gani? Labda ni Mungu wa kichina.Sio Mungu wa Israel aliye hai.

      Delete
  6. ACHA KUWATUKANA WATUMISHI WA MUNGU WEWE UNAYECOMMENT KITU USICHOKUWA NA UHAKIKA NACHO USIJE UKAPATWA NA MADHARA MAZITO BAADAYE UKAJUUTA! KAKOBE NI MTUMISHI WA MUNGU ANAYEHUBIRI UTAKATIFU KWA GHARAMA YOYOTE.JE KUNA MCHAWI ANAHUBIRI WATU WAACHE DHAMBI /WAOOKOKE? FUNGA MDOMO WAKO!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtunishi gan mwiz tu huyo,toto lake vuta bangi kashindwa kuliombea!

      Delete
  7. Ubunge wenyewe kapewa tu........

    ReplyDelete
  8. Pumbavu mtumishi my ass mmeshalogwa huko mnanyenyekea MTU kuliko mungu yatatupata yapi hayo?

    ReplyDelete
  9. Hakuna dhambi mbaya kama kuwanenea watumishi wa Mungu uongo, na alaaniwe yeye amuhukumie jirani yake,. Kakobe ana waamuin kama zaman kama wewe ulikimbia ni wewe kwasababu unapenda dhambi,. na kuhusu kuvaa kilemba kwa wanawake ni lazima, soma corinth utaona, na kuhusu mtoto wake kunywa pombe ujue shetani ameshndwa kuingia kwa wazazi kwa sababu ni watakatifu so anapitia kwa watoto.

    ReplyDelete
  10. Wote wanaomtetea kakobe ni misukule yake .

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad