NECTA Yabadilisha Viwango vya Ufaulu Form 6, DIV I Mwisho point 7

NECTA imetoa mwongozo wa matumizi ya viwango vya Ufaulu (Aprili 2014) ambao umesambwazwa katika shule zote ze sekondari kupitia kwa Maafisa Elimu wa Mikoa. Kwa mujibu wa mwongozo huo Madaraja ya ufaulu kwa Kidato cha Sita 2014 yatapangwa kwa kutumia mfumo uliooneshwa kwenye ukurasa wa 8 wa mwongozo huo ambao ni:
Div I pointi 3-7
Div II pointi 8-9
Div III Pointi 10-13
Div IV awe na D mbili au C moja
Div 0 aliyepata chini ya D mbili.

Kwa mujibu wa mwongozo huo masomo yatakayohesabika kwenye kupanga pointi ni yale tu yaliyoko kwenye tahasusi yaani combination. Kwa maneno mengine suala la kupata cheti kwa mgongo wa Bible Knowledge au Islamic Knowledge litakuwa halipo tena.

Kuanzia Kidato cha Nne 2014 na Kidato cha Tano Sita 2015 mfumo wa GPA utatumia. Kwa maelezo Zaidi soma kurasa wa 8 na 9 na pia unaweza kukipata kijitabu hicho toka shule yoyote ya sekondari au kwenye ofisi za elimu za mkoa na wilaya.
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sasa wanataka kuua watoto kupata cheti hapo issue..bora ukimaliza form 4 ukachukue certificate tu na diploma ndio uhakika

    ReplyDelete
  2. Hello hello Tanzaniaaaa, Tuimbeeeee.!!

    ReplyDelete
  3. Naipongeza serikali kwa hilo ili kuondoa vilaza mashuleni

    ReplyDelete
  4. That is a great motion, big up necta

    ReplyDelete
  5. Utawaua wale watoto wa masheikh maana shule zao zinategemea Islamic knowledge kupata div 1. Duh noma sana hii mpya...

    ReplyDelete
  6. Utawaua wale watoto wa masheikh maana shule zao zinategemea Islamic knowledge kupata div 1. Duh noma sana hii mpya...

    ReplyDelete
  7. Tuimbeeeeeeeee......TZ @50

    ReplyDelete
  8. hizo grade kubwa sana....watoto watafeli sana hasa hasa kwa advance.....advance level ya TZ ni ngumu sana compared to other countries...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad