Ni wazi kwamba katika maisha ya mwanadamu, mara nyingi kila mtu anakuwa na mtu fulani anayemvutia kwanye mambo fulani fulani na kumfanya anayevutiwa kupenda kuiga toka kwa yule anayetenda "Role Model".Katika siasa wapo watu wa namna hii vile vile ambapo wadau na wanasiasa wanaochipukia hutamani kuwaiga!.
Binafsi kwa hapa Tanzania; Katika medani za siasa, 'Role Model' wangu ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete!. Mwanasiasa huyu amekuwa akinivutia zaidi katika jambo moja kubwa: Jinsi anavyoshughulikia migogoro ya kitaifa na kimataifa.Mh. Kikwete amekuwa anaonesha uwezo mkubwa katika kuepusha migogoro (hasa ya kisiasa), na inapotokea mgogoro umeibuka, amekuwa anaonesha umahiri mkubwa kuidhibiti kwa kutumia mbinu za kistaarabu kabisa na inapobidi kuitatua; basi amekuwa akiitatua kwa njia za kidiplomasia (mifano ni mingi mno).Kimsingi binafsi navutiwa sana na kiongozi mwenye uwezo mkubwa wa kutatua migogoro kwa njia ya diplomasia.Naweza kusema Rais Kikwete ndio Mwanadiplomasia bingwa wa zama hizi katika eneo letu hili la Afrika Mashariki na kati.
Awali nilidhani kwamba niko peke yangu ambaye ninamtazama Mh.Kikwete kama 'role model' lakini baadae niligundua kwamba tuko wengi.Kwa mfano Mwaka 2012 mkoani kilimanjaro, Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Mbowe alisema;
"Nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - (Freeman Aikaeli Mbowe, Nov 2012) Hii ni wazi kwamba kumbe tuko wengi tunaomuhusudu huyu Mwanasiasa!
Any way! wewe ndugu yangu sijui "Role Model" wako ni nani katika siasa za Tanzania? na kwa nini?
N.B
Kama mtu ukisoma hii mada huelewi ni bora usichangie! unaweza kusoma tu michango ya wenzako kuliko kutoa matusi humu!
Halima Mdee! Yuko Smart kiufahamu.
ReplyDeleteJulius Nyerere
DeleteEdward lowasa , Huyu bwana ni mtu wa vitendo
ReplyDeleteEsta Bulaya,sio mnafiki,sio mbinafsi,anasaidia vijana,ni kama marehemu Amina chifupa.
ReplyDeleteBulayo na Lowasa ni "perfect role model in tz politics"
ReplyDeleteNyoooo admin.mshenz mbon habar nyengin huwaambii watu wactukane umewaambia hii tu unawazime ww
ReplyDeleteUmekuwa bias sana kama vile unampigia chapuo mkuu wa kaya.wewe ungeiacha mada wazi watu wachangie.usingeweka picha ya rais.
ReplyDeleteTanzania nzima hakuna kama mohammed dewji , tuache kusifia jamani tuseme ukweli
ReplyDeleteNa wewe umevulugwa nini?sasa dewji kafanya siasa gani kwa mfano?
DeleteMh. Tundu Antipas Mwigayi Lissu.anajenga hoja sana na anajua vifungu vingi vya sheria.ananipa raha akiwa anajenga na kupangua hoja kwa facts.
ReplyDeleteYes yes! Tundu Lissu ni alfa na omega !Tanzania ya leo inahitaji mwanasiasa asiyejua kuremba na jasiri kama Lissu.
ReplyDeleteOle sendeka mwamba ule usioteteleka
ReplyDeletetundu lisu kidume
ReplyDeleteTundu Lisu, oyeeeeeeeeeee!
ReplyDeleteEmphrem polepole ..yupo fresh
ReplyDelete