Huku majirani na watu wengine wakishangazwa na kitendo hicho, Anord alimfungia ndani baba yake mzazi na kuanza kumshambulia kwa silaha mbalimbali kabla ya kuchukua panga kwa lengo la kutaka kummaliza kabisa.
Mzee Michael, kuona kijana wake amepania kummaliza, alipiga mayowe ya kuomba msaada, kitu ambacho kilifanikiwa kwani mara moja wasamaria wema walijitokeza na kumuokoa kwa kumhifadhi katika chumba kingine ndani ya nyumba hiyo.
Pamoja na hivyo, kijana huyo ambaye bado watu wana mashaka na utimamu wa akili yake, aliendelea kufanya fujo huku akivunja mlango wa chumba alichohifadhiwa baba yake ili aweze kumtoa roho, huku pia akitishia kumuua mtu yeyote ambaye angejaribu kumsogelea.
Baba Aliyetaka kuuwawa |
Akiwa katika hatua za mwisho kuvunja mlango huo huku baba yake naye akianza kusali sala ya mwisho kabla ya mauti kumfika, ghafla askari wenye silaha waliwasili eneo hilo na kuanza kumdhibiti kijana huyo.Hata hivyo, zoezi la kumdhibiti kijana huyo halikuwa rahisi, kwani bado alisababisha timbwili kubwa kabla ya maafande hao kutumia ujuzi wa kikazi bila kutumia risasi na kumweka chini ya ulinzi.
Katika hali ya kushangaza, baada ya askari polisi kumuuliza sababu iliyomfanya afikie uamuzi wa kumuua baba yake mzazi, Anord alidai mzee huyo ndiye chanzo cha yeye kuharibikiwa kimaisha.
Baadaye maafande hao walimzoa kijana huyo na baba yake kuelekea Kituo cha Polisi Mabatini Kijitonyama kwa mahojiano zaidi.
Bangi hizo
ReplyDeleteAmefanya aharibikiwe kimaisha kivipi?????.....kama kweli huyo mzazi angetaka aharibikiwe kimaisha huyo mtoto angekuwa hai mpaka wa leo hii??????......mijitu mingine bwana. Mtoto achana na uzembe. Hizo nguvu ulizokuwa nazo za kumpiga baba yako kazitumie kufanya kazi.
ReplyDeleteMajanga
ReplyDeletehmmm shughuli kazi hiyo haya sasa mitpto kama hii iwe kumi, utasema una watoto mitoto mboni balaa manake ata yule mwenye mtoto mmja mwenye akili atasema ana mtoto, kuliko mitoto kumi kama hili, kwanza nashangaa familia zingine toto kama hili lianzage huko likatafute maisha yake jitu kubwa jinga tu lataka kulishwa, mishwaini mijitu ya dizaini hii, ndio maana anataka mtoa roho baba yake, ili ajinafasi kwa mali asiyo itolea jasho
ReplyDeletekazi kwelikweli
ReplyDeleteWasio na watoto wanalilia kupata watoto, wenye nao wanataka kutolewa uhai. Mungu tuepushie vizazi vyetu. Sasa wewe anorld ukimuua babako ndo utafanikiwa? Tubu kwa Mungu na babako pia la sivyo utaharibikiwa zaidi.
ReplyDeleteIngekuwa sisi wakurya huyo mtoto angeozea jela, sisi hatubembelezi motto ila baadhi ya makabila mengine wanawachekea watoto. Pia wanaukoo wangemtandika viboko ambavyo asingevisahau maishani mwake. Hoyu motto hakukurupuka tu alianza kudekezwa kidogokidogo mpaka kufikia hatua ya kujiona ana haki na mali asiyoitolea jasho..
ReplyDeleteBangi za kukopa izooo
ReplyDeletehuyo mtoto ni msenge apelekwe selo akabakwe kiduchu
ReplyDeleteWatoto wa hivo, unamtoa kafara, unakula pesa, kumaliza ma blaa
ReplyDelete