Sakata la Mawaziri Mizigo Laibuka Tena....Wajipanga Kujitetea

Stori: Mwandishi Wetu, Dodoma
SAKATA la mawaziri kutajwa kuwa ni mizigo, lililoibuliwa kwa mara ya kwanza na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, limeibuka tena mwishoni mwa wiki iliyopita na kusababisha viongozi hao kujipanga ili kujitetea, ndani na nje ya Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma.
Wakati Nape alirudia kauli yake hiyo kwa mara nyingine wiki iliyopita mjini Igunga, Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola naye alimwita Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza kuwa ni mzigo kwa kitendo chake cha kushindwa kuwajibika, hasa katika sakata la mbegu za pamba.

Habari kutoka kwa watu walio karibu na mawaziri wanaotajwa kuwa ni mizigo, zinasema ili kuhakikisha hawapati shinikizo kama ilivyokuwa mara ya kwanza, wamejipanga kujitetea kwa nguvu zote, ndani na nje ya Bunge, kwa kigezo kuwa wanaopiga kelele dhidi yao, wanatumiwa na wapinzani wao kisiasa majimboni.

“Hali siyo nzuri kabisa kaka, wameshtukia kuwa kuna njama za makusudi za kuwang’oa, wanataka kutumia hii nafasi kujinasua, kwa hiyo kuna mikakati inapangwa kuonyesha kuwa kelele dhidi yao zina mkono wa wapinzani wao kisiasa, wanadai hata wanaopiga kelele kutoka CCM, nao wanatumiwa,” kilisema chanzo hicho.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Serikali ya ccm yooote ni mzigo,hakuna asiyekuwa mzigo,kwa hiyo kuitana mizigo ni usanii tu wa kuendelea kudanganya wad(t)anganyika na kuwapumbaza eti ccm wana jipya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni mizigo kuanzia rais na viongozi wooote kuma nina zao!

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad