Sasa ni Wakati wa Wachezaji wa Taifa Stars Kuwafuta Machozi Watanzani

Na Baraka Mbolembole
Brazil inaweza kuwa nchi pekee katika soka ambayo waandishi wake wa habari wanaweza kuungana na wachezaji katika kushangili ushindi wa timu na kuhoji wachezaji inapotokea wachezaji hawajitumi ipasavyo uwanjani. Waandishi husimama kando ya uwanja dakika chache kabla ya kuanza kwa mchezo kuhoji wachezaji kabla ya kuanza mchezo,wakati wa mapumziko na wanapotolewa uwanjani baada ya kupewa kadi nyekundu.
Kwetu sisi, sirahisi sana kufanya hivyo ila bado Watanzania wanapata taarifa zote muhimu kuhusu timu yao ya Taifa kwa kila matukio yanayokuwa yakijitokeza, iwe kwa matukio mazuri au mabaya. Hii ni sababu kubwa ya kuamini kuwa vyombo vya habari nchini vipo nyuma ya timu yao yaTaifa na mara zote vinapenda kuona mafanikio ya kipatikana. Hatutaacha, bado tunaendelea kupamba na katika kuiunga mkono, Taifa Stars na siku yajumapili, tutakuwa nyuma ya kikosi hicho ambacho kitaikaribisha timu ya Taifa ya Zimbabwe katika uwanja waTaifa katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa AFCON 2015, Morocco.
Kocha wa timu yaTaifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mholanzi, Martin Nooij amempatia nafasi ya jukumu la Unahodha wa kikosi hicho mlinzi wa kati, Nadir Haroub, huku mlinzi mwingine wa kati, Aggrey Morris akiwa kaimu nahodha wa timu hiyo ambayo itacheza na timu ya Zimbabwe katika michezo miwili ya mtoano kuwania kufuzu katika hatua ya makundi kuwania nafasi ya kufuzu kwa michuano ya AFCON 2015, Nchini, Morocco. Nadir amejiimarisha na kuwa mcheza bora kwa mara nyingine baada ya kuanza msimu uliopita kwa kusuasua, amesisimua kwa uchezaji wake katika raundi ya pili ya lig ikuu Tanzania, na kitendo cha kurudishwa ghafla kikosini, Stars kinaweza kutoa wazo mbadala kwa makocha wapya, Nooij, na Salum Mayanga la kuunda upya safu ya ulinzi ulinzi katika mechi hizo muhimu kwa timu ya Tanzania..
Katika michezo miwili dhidi ya Al Ahly, Nadir, alicheza kwa kiwango kilichostahili kiasi cha kukumbusha enzi zake akiwa roho ya safu ya ulinzi ya Stars chini, Marcio Maximo. Alikuwa bora katika michezo yote miwili ya klabu yake dhidi ya waliokuwa mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri katika michuano ya klabu bingwa, sawa na alivyocheza katika ligi kuu, raundi ya pili. Kama alimudu kucheza vizuri mechi ya Afrika iliyoshirikisha klabu bora, anastahili kuvaa jezi ya Stars dhidi ya Zimbabwe.
Tanzania haina uhakika kama itawaondoa, Zimbabwe, timu hiyo ina washambuliaji wakali. Tofauti na ilivyokuja, novemba, 2013, katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki,safari hii, Zimbabwe itakuja, Tanzania na kikosi cha kupamba na huku, Knowledge Musona akiongoza safu ya mashambulizi. Wachezaji, Nadir, Aggrey, Said Mourad, Kelvin Yondan wanatosha katika nafasi ya ulinzi wa kati. Awali, Nadir alitemwa kwasababu za kisoka, na sasa ni sababu hizo hizo zimemrejesha na kumpatia ‘ beji ya unahodha’. Beki huyo aliyeiwakilisha, Tanzania katika michezo 35 na kuifungia goli moja, alipangwa pamoja na Aggrey katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Malawi, siku ya jumapili iliyopita na walicheza vizuri.
Nadir, amepevuka vya kutosha kwa sasa katika mchezo wake. Safu ya ulinzi ya Stars chini ya Shomari Kapombe, Nadir, Aggrey na ErastoNyoni, ilifanya kazi nzuri kwa dakika zote dhidi ya Malawi katika mchezo uliomalizika kwa suluhu-tasa, kuliko vile walivyocheza na Burundi na kuchapwa magoli 3-0, siku kumi zilizopita. Walijipanga vizuri, walikuwa imara na hawakutoa nafasi kwa washambuliaji wa Malawi. Stars ilikuwa imara katika ulinzi kutokana na uwezo wa mabeki wa kati na wale wapembeni. Kurejeshwa kundini kwa Yondan ni jambo zuri kwa kuwa mlinzi huyo ana uzoefu wa kutosha. Nooij, anaweza kufanikiwa katika malengo yake ya kuipaisha, Stars kama wachezaji wazoefu waliopo watajitoa kwa timu.
Zimbabwe ni timu, si ngeni kwa wachezaji wa Stars, hivyo wanatakiwa kupokea mafunzo ya walimu wao kwa uhakika ili kuweza kufuzu katika kundi la tano, ambalo tayari timu za Zambia, Cape Verde na Niger zimefuzu moja kwa moja. Nahodha huyo mpya wa Stars ameonekana kuhamasika na jukumu hilo
Kama, wachezaji wazoefu watacheza kwa kiwango kizuri timu itanufaika na uzoefu wao, ila endapo wataendelea kucheza kwa viwango vilevile vya siku zote, hakutakuwa na kipya katika timu hiyo na Nooij ataanguka kama ilivyokuwa kwa, MarcioMaximo, Jan Poulsen na KIM. Japo kuwa tumewalaumu makocha wote waliopita, kuwa hawakuwa na mbinu nzuri za kuipandisha Stars, ukweli walijitahidi lakini wakaangushwa na baadhi ya wachezaji muhimu ambao waliwekeza mbinu zao kwao. Nooij, amejipa mwenyewe alama ya mapinduzi, Malinzi amesema kuwa hakuna mtu atakayemuingilia katika uteuzi wa wachezaji, sasa ni jukumu la wachezaji kuamka na kuaminiwa na wanaweza kufuzu kwa fainali za Afrika.
Siku 13 kabla ya kuivaa, Zimbabwe, kocha wa Stars, Nooij alisifu namna timu yake ilivyoweka mpira chini dhidiya Malawi, ila amelalamikia upotezaji wa nafasi za kufunga ambazo wachezaji wake walizipoteza katika mchezo huo. Chini ya mwalimu, Maximo, Stars ilikuwa ngumu kufungika, ukitoa kipigo cha Dakar, Stars haikufungwa magoli zaidi ya mawili katika mechi moja katika michezo ya mashindano. Maximo alipata bahati ya kufanya kazi na wachezaji wenye nidhamu kubwa, Shadrack Nsajigwa, Mecky Mexime, Salum Sued, Nadir, Erasto Nyoni, na Victor Costa. Hawa ndio walinzi walioifanya Stars kuwa ngumu kufungika chini ya Maximo, walikuwa wakicheza kwa kujituma na nidhamu, walisumbuliwa na tatizo la kukosa umakini ila usingeweza kufunga magoli matatu. Alipokuja, Jan, kisha KIM, Stars imekuwa ikifunguka na kucheza kwa kushambulia zaidi. Kocha mpya atakuja na mfumo gani?
071408 43 08
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tulishakua kichwa cha mwendawazimu, zimbabwe watatufumua vizuri tu kama wananawa

    ReplyDelete
  2. sometime we have to accept and respect the expert of our coach otherwise we shall not succed

    ReplyDelete
  3. sometime we have to accept and respect the expert of our coach otherwise we shall not succed

    ReplyDelete
  4. kesho ndo tutajua uwezo wa uyo coach, tatizo soka letu pia limejaa siasa... Mpira wa magazetini

    ReplyDelete
  5. kama yanga vile

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad