Snura Aingilia Kati Beef la Wema Sepetu na Kajala

  MSANII wa filamu na muziki, Snura Mushi ameingilia kati ugomvi wa wasanii wenzake, Wema Sepetu na Kajala Masanja na kuwaagiza wamalize tofauti zao.

Wasanii hao ambao wameingia kwenye bifu la kufa mtu kufikia hatua ya kuanikana kwenye vyombo vya habari huku chanzo kikubwa kikitajwa ni shilingi milioni 13 ambazo Wema alimlipia Kajala kama faini ya kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa rehani kisheria iliyokuwa ikimkabili mahakamani.

Nyumba hiyo iliwekwa rehani kutokana na mume wa Kajala, Faraja Agustino kushitakiwa kwa kosa la kutakatisha fedha haramu.

Snura amewataka Wema na Kajala kutoangalia nani ana makosa, wamalize tofauti zao.
“Nawashauri wenzangu wasigombane na kuwekeana vinyongo hiyo ni kama wanawapa watu faida,

nawaomba wamalize kwani haipendezi kabisa kwa jinsi walivyokuwa wameshibana. Kama mmoja anaona amemkosea mwenzake ajishushe na kuomba msamaha,” alisema Snura.
By Na Chande Abdallah na Mayasa Mariwata GPL

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sipendi unavyokatika hovyo kanda zako ukiwa na watoto wala huangali unanikera badilika hata kama ndio inakupatia soko na money but act like a lady miuno kama kanga moko inachefua

    ReplyDelete
  2. kweli mdau linakatika kimalaya sana.. kuimba kwenyewe hajui so anakata mauno auze vizuri k yake

    ReplyDelete
  3. Hahaaaa haya snura unaloambiwa nikweli cheza kwastaha sio kichumbani

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad