Steve Nyerere:Mimi ni Kiongozi na Mfano wa Kuigwa Nimemaliza Bifu na Batuli

Stori: Gladness Mallya

IMEKAA poa sana! Lile bifu lililotia fora kwa wasanii wa filamu, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ huku kila mmoja akiapa kutopatana na mwenzake, hatimaye limekwisha siku chache baada ya kifo cha msanii mwenzao, Adam Philip Kuambiana.

Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao walimaliza tofauti zao kutokana na kifo cha ghafla cha Kuambiana hivyo wakaamua wenyewe kuyamaliza kwani wameona maisha ni mafupi.
“Steve na Batuli kwa sasa wameshamaliza tofauti zao, wamepatana, wanaelewana vizuri sana na ni baada ya kifo cha Kuambiana ndipo walikaa wakaamua kuzungumza na kumaliza tofauti zao,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Ijumaa Wikienda liliwasaka wahusika ambapo Batuli alithibitisha kwamba ni kweli amemaliza tofauti zake na Steve na sasa wameanza maisha mapya kwani amegundua maisha ni mafupi na kifo kinakuja muda wowote.

Kwa upande wa Steve Nyerere alikuwa na haya ya kusema: “Mimi ndiye Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity na nilishasema nitamaliza tofauti zote yaani mabifu yote yataisha kwa sababu mimi ni kiongozi na mfano wa kuigwa nimemaliza bifu na Batuli naamini na hayo mengine yataisha, huu ni mwanzo tu.”

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ingekuwa ww kiongozi wa kuigwa ht hilo bifu lisingekuwepo kabisa kwa nini mwanzo mliliruhusu likawepo?ww sio kiongozi wakuigwa ht kidogo unawagawa wasanii kwnye msiba makundi makundi nani aige upuuzi wako huo?kwanza kiongozi gani ww wakati jb kaenda uturuki ulitangaza bifu nae akirudi kisa hukuchaguliwa na ww huna lolote kwenda zako we mshamba tu

    ReplyDelete
  2. steve mshamba na cjui kwanini watu walimchagua uyu ndo matatizo ya bongo movie

    ReplyDelete
  3. Halafu huyu jamaa anapenda kupiga virungu viongozi kwa kujikombakomba huyu balaa

    ReplyDelete
  4. mbona yuko fresh

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad