Sumatra Yafunga Kituo cha Daladala Mwenge D’Salaam

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imetangaza kuhamisha kituo maarufu cha daladala cha Mwenge kwenda eneo la Makumbusho.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, ofisa mfawidhi wa Sumatra wa Kanda ya Mashariki, Conrad Shio alisema Kituo cha Mwenge kitafungwa rasmi Jumapili na eneo hilo litabaki wazi kupisha upanuzi wa Barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Shio alieleza sababu ya kuhamisha kituo hicho kuwa ni ufinyu wa eneo lenyewe jambo linalosababisha magari kushindwa kuingia kituoni hapo kwa wakati, hasa nyakati za asubuhi na jioni. Hali hiyo husababisha foleni kubwa isiyo ya lazima.

Alisisitiza madereva wote kutii agizo hilo kuanzia Jumatatu na kwamba atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria. Pia, aliwataka abiria kutolazimisha kushushwa katika eneo hilo wakati hakuna kituo. Shio aliongeza kuwa barabara za kuingia na kutoka Kituo cha Makumbusho bado zinakarabatiwa na Manispaa ya Kinondoni ili kurahisisha uingiaji na utokaji wa magari katika kituo hicho.

Hivi karibuni, madereva wa daladala zinazofanya safari kati ya Mwenge, Tegeta na Ubungo waligoma kutoa huduma kushinikiza Serikali kueleza kituo mbadala baada ya kufungwa kwa kituo cha Ubungo kutokana na ujenzi unaoendelea wa barabara.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Completely nonsense.

    ReplyDelete
  2. Ni sawa lakini mjue nakutengeneza barabara hamuonagi aibu mnapokwenda kwa nchi za wenzenu

    ReplyDelete
  3. hizo barabara zenyewe zinazojengwa na magufuri hazina ubora wowote. bunge limempa pesa nyingine akazitafune

    ReplyDelete
  4. jaman sasa kwamie nashukia itv, ntafanyaje... Na barabara zenu toka muanze ujenzi hamna hata moja iliokamilika....

    ReplyDelete
  5. Naikamilika haina ubora ikija mvua ya wiki tu zote znasombwa namfuriko.maanina kuleni helasana nanyie mtaliwa tu malipo duniani ahera yaenda hesabu.

    ReplyDelete
  6. dah nna mawazo na rais ajaye cjui nae ndo majanga zaid ya haya.. Lol

    ReplyDelete
  7. Km kuna ujinga nlowah kuuckia ni huu wa kuhamisha kituo cha mwenge!! Pale ndo junction tena rahic kwa kuingia na kutoka!! Tyr eneo la makumbusho lina folen asbh na jioni ss ongezea na turning ya daladala zote itakuwa hapo!!!
    Cjaona udogo wa brbr ya Ali Hassan Mwinyi eneo hlo unasbbsha kuhama kwa hcho kituo!!! Tunaoishi Mwnge tukitaka kwenda posta au kkoo ndo kutembea mpk makumbusho!!!
    Nosense everywhere

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad