Taifa Stars Mmefanya Vizuri Ila Hongera Yangu Siwapi Leo

Leo Team ya Mpira ya Taifa ijulikanayo kama Taifa Stars ilikuwa inapambana na Team ya Taifa ya Nchi ya Zimbabwe na Matokeo ni Taifa Star imemaliza mechi na Ushindi wa Bao Moja Katika Mchezo huo wa kwanza ya raundi ya awali ya kugombea kwenda AFCON 2015 .Nadiriki kusema kuwa Taifa Star walikuwa na Nafasi kubwa sana ya kushinda Mechi ya Leo zaidi ya Mabao matatu kwa Kuwa walikuwa Nyumbani na jinsi nilivyouangalia Mpira lakini ilishindwa kuendeleza kasi waliyokuwa nayo mwanzo , Bao moja si baya ila kumbuka tuna mechi ya marudiano ambayo itafanyika Zimbabwe siku za Karibuni, So tungewafunga mengi tungejiweka nafasi nzuri ya Kushinda...Kule kwao tunahitajika tutoke Droo ama tuwafunge ...So Hongera yangu nitawapa siku nkiwafunga Zimbabwe kwao...
Toa Maoni yako 
Udaku Sports

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad