TAKWIMU ZA NGOMA (UKIMWI) HIZI HAPA, MIKOA INAYO ONGOZA TANZANIA

Cha ajabu mkoa wa Tanga ambao watu wanadai wapo vizuri kweye swala zima la mapenzi maambukizi yapo chini! Do they play safely? Manyara pia! Pemba na Zanzibar ambako watu wanadai kuna mapinduzi ya mapenzi nako maambukizi yapo chini! How this is possible?

MSEMAJI wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Glory Mziray hivi karibuni alisema Mkoa wa Njombe, Mbeya na Iringa ni vinara wanaoongoza kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini.

Alisema Njombe inaongoza kwa asilimia 14.8 ikifuatiwa na Iringa kwa asilimia 9.1 na Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya tatu kwa asilimia 9.

Mikoa mingine na asilimia za maambukizi katika mabano ni Ruvuma (7.2), Shinyanga (7.4), Dar es Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi (5.9), Pwani (5.9),Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita (4.7).

Mikoa mingine aliyoitaja ni Mara (4.5), Mwanza (4.2), Mtwara (4.1), Kilimanjaro (3.8), Kigoma (3.4), Simiyu (3.6), Morogoro (3.8), Singida (3.3), Dodoma (2.9), Manyara (1.5), Lindi (2.9), Tanga (2.4), Unguja (1.9) na Pemba (0.3).

Mziray alisema takwimu hizo zinatokana na utafiti uliofanyika mwaka juzi hadi mwaka jana. Kutokana na matokeo hayo, alisema maambukizi ya Ukimwi yamepungua kwa kasi ndogo.

Alisema Watanzania walioonesha kuwa na ufahamu sahihi wa elimu kuhusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi wanafikia asilimia 60 jambo linalosababisha kuwepo mwamko mdogo wa kubadili tabia.

Kuhusu tohara kwa wanaume, alisema inapunguza maambukizi ya Ukimwi kwa asilimia 60 na kusisitiza kuwa ipo haja ya kutoa elimu zaidi juu ya uelewa wa ugonjwa huo.

Visababishi vya Ukimwi:

Miongoni mwa vipengele muhimu ni pamoja na vifuatavyo:


Uasherati
Matumizi madogo na yasiyo endelevu ya kondomu
Ngono za marika yanayotofautiana sana
Kuwa na wapenzi wengi.
Ukosefu wa elimu ya maambukizo ya UKIMWI
Kuwepo kwa maradhi mengi ya ngono kama vile tutuko, homa,
Jando kwa wanaume


Sababu za mahali husika, za kushamiri kwa janga nchini ni:


Umaskini na biashara ya ngono pamoja na ongezeko la wafanyabiashara wa ngono
Tabia mbaya za ngono za wanaume kutokana na kuruhusiwa kimila kuwa na nguvu
Kukosekana usawa wa kijamii, kiuchumi, kisiasa na kijinsia pamoja na unyanyaswaji wa wanawake na wasichana walio ndani na nje ya mahusiano.
Matumizi ya pombe na dawa za kulevya.
Tabia za kimila (kama vile utakasaji wajane na jando na unyago)
Safari za aina zote zinazosababisha kuwa mbali kwa wanandoa na ongezeko la mahawara
Kutokutahiriwa

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tusipobadirika na kumrudia Mungu yataongezeka wala si kupungua maana wenye UKIMWI na wanatembea nao bado hawajapima ni wengi mno. Tukimrudia yy atatusamehe.

    ReplyDelete
  2. Kwani Unguja na Pemba ni Mkoa enhe? Ndio maana hawataki Muungano na Ujinga wenu nyie Watanganyika

    ReplyDelete
    Replies
    1. ulitaka ziitwe nchi ya unguja na nchi ya pemba?

      Delete
    2. Walitakiwa kusema visiwa na ukiitizama lindi,tanga,pemba na unguja nizamu za zinaaa ni ndogo watu wanadini za kufuata na watu wanatahiriwa ni wengi wanapofanya mapenzi hujitia maji na wakimaliza maji janaba kuoga sio uchafu uchafu tu elimu muhimu ya dini. Hapa kwetu dar es salaam watu wamepaharibu mpaka hata maana halisi ya neno waswahili imepotea neno waswahili imekuwa ni watu Wenye tabia mbovu na za ajabu rudi 70's utajua maana ya waswahili. Ila huu ugonjwa japo sio wote wanapata kwa uzinifu lazima tanzania wawe makini na elimu na waache kutangazia zinaaa matangazo condom condom ndio Kama kusema fanyeni tu zinaa zenu Wenzenu wanauza biashara tanzania inaangamia kwa zinaa.

      Delete
  3. muungano wa nini kwan wale makupe 2, tuwe makin na ukimwi jaman

    ReplyDelete
  4. AIDS has no cure till this moment, guys take care!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mungu ameweka kila gonjwa Lina dawa kuijuwa tu dawa yake ya sasa hivi kuwacha zinaa watu kujiheshimu na maaadili nchi Ina promote sana uzinifu hii.

      Delete
  5. Mw. Mungu tupe mwisho mema

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad