Najua ni mapema sanaaa yani kuwaza habari za mapenzi asubuhi yote hii,ila mara moja moja si mbaya....
Okay back to topic.....
Hii ya leo inawahusu wanaume mliooa au ambao mko engaged kuelekea ndoa,vijana ambao bado mna chagua chagua tafadhali acheni kaka zenu waseme au mkisema basi muwe mnasema ya kweli....
Swali ni hivi....NINI KILIKUFANYA UMCHAGUE MKE/MCHUMBA ULIENAE??...what made you conclude she is the one?...sababu zipi yani,uzuri wake,sura,umbo,tabia,elimu,kip ato?au ulimpa ujauzito au ulijua tangu siku ya kwanza umemuona au??au kuna situation flani ilitokea ndo ukajua ndo yeye...au?.....au?.....
mi sijui,naomba mtuweke wazi mkiambatanisha na mifano 'practical' kabisaaa itakuwa poa zaidi....
Mind you,utakaposema hapa utamsaidia rafiki yako ,mdogo wako ama ndugu yako kupata uelewa yakinifu kuhusu wanaume linapokuja swala zima la ndoa.....mana kama mjuavyo waliozidiwa desperado wanazinatafuta hadi kwa waganga eti hhehehe...naamini hii ishu haina uchawi yani...
Karibuni sana kwa michago,kejeli si mpango,vichekesho ruksa......
1 hakuonyesha tamaa ya pesa,alikuwa anahamasha kuweka akiba kuliko kutumia 2 aliniheshim Mimi pamoja na ndugu zangu 3 hajajichubua 4 mcha mungu
ReplyDeleteMimi nilichagua kwa kuangalia tabia yake kiujumla. Yaani anaheshima kwangu na ndugu, tunasikilizana na kuelewana, alikuwa na malengo ya kujieldeleza kielimu na uchumi.
ReplyDeletemim nafkikri silaha kubwa ya mwanamke ni uadlifu sababu ni kila kitu kwa mfano mama kwenye familia akichepuka inakuwa aibu kubwa kuliko baba akifanya hvyo hii ni kwasababu mama ni msingi wa uadilifu na heshima ndani ya nyumba!hilo ni moja jingine ni namna ambavyo msichana anajihusisha na marafiki zake kama uko naye na anawashirikisha kwa kila jambo na ukigundua kuwa maaumuzi yake huwa yanatoka kwa wenzake huyo sio mke.
ReplyDelete