Upinzani Watoa Masharti Magumu Kushiriki Uchaguzi Mkuu 2015

Serikali imetakiwa kuandaa taratibu za mpito za kushughulikia Uchaguzi Mkuu ujao ili kunusuru nchi kuingia katika mtanziko unaoweza kuwa chanzo cha machafuko ya kisiasa, endapo utafanyika bila kupatikana kwa Katiba Mpya la sivyo Kambi Rasmi ya haitashiriki.
Hayo yalielezwa jana na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alipokuwa akitoa hotuba ya kambi hiyo bungeni kuhusu Makadirio ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

“Hatuwezi kuingia uchaguzi wa vitongoji, vijiji na mitaa kwa utaratibu uliopo leo, hatuwezi kwenda kwenye Uchaguzi Mkuu mwakani na Tume ya Uchaguzi kama ilivyo leo, hatuwezi tena kwenda kwenye Uchaguzi Mkuu mwakani wakati matokeo ya uchaguzi wa Rais hayawezi kuhojiwa mahakamani.”

Aliongeza: “Hatuwezi kuingia kabla na hoja ya mgombea huru haijapatiwa majibu, tukiwa na daftari la wapigakura lililopo leo na hatuwezi kulikubali daftari jipya litakalotengenezwa kama wadau wote hatutashirikishwa kikamilifu.”

Kauli hiyo ya Mbowe imekuja siku moja tu baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwasilisha bungeni, Bajeti ya ofisi yake ambayo imetenga Sh5 bilioni kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Mbowe alisema kama ilivyo kawaida, Serikali na CCM inaweza kupuuza tahadhari hizo na kulazimisha kwenda katika chaguzi hizo katika mazingira ambayo hayana mwafaka kama inavyoonekana sasa katika Mchakato wa Katiba Mpya.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. yani nyie mnataka kuwapeleka peleka watu wawasikilize nyie tu, mara leo hivi, kesho hivi, ilimradi tu tafrani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kaa kimya huna unalolijua kuhusu nchi hii wewe subiri uchaguzi unakuja utapewa tshirt yako na pilau na sukari halafu utapanga folen kwenye jua kali ili uwape tena mafisadi waendelee kukunyonya maskini wewe.

      Delete
  2. Katiba nchi hii akuna. Kama ninyi wrote mnaojiita wadau au mnauchungu Wa nchi hii yaTzn basis msiende bungeni kuchukua posho. Mnasema mnauchungu name nchi hii lakini mnakubali kupoteza kula Siku tsh m200. Arafu hoo Mimi nawatetea wtz .kama kweli mnauchungu name hii nchi mkienda Dodoma binge la katiba msilipwe posh name hizo posh ziende kwenye mahospital name maswala mengine yanohusu wananchi. Badara take make kwenye maema name kipikwe chakula cha pamoja Harpo ktba itapatikana safi. Nyinyi wrote waongo mnatafuta pesa Anna data mmja anaewajari wtz

    ReplyDelete
  3. nimekuelewa mchangiaji hapo juu... wana siasa wote wanatoka kiwanda kimoja tofauti yap ni matangazo yao ya biashara tu.. hao ukawa wanalazimisha inchi iingie kwenye machafuko huku watoto zao wanaishi marekani na uingereza...
    hatutaki upumbavu wenu mmegomea katiba leo mpo kwenye bunge la bajeti sasa maana yake nini.. stupid

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe bunge la bajeti na katiba ni vitu viwili tofauti!jaribu kufuatilia vizur mustakabari wa nci yako ndio utajua mbivu na mbichi!bado bonho lala wewe.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad