Video Mpya ya Mwasiti “Serebuka” ilivyosababisha Gumzo Kubwa Kuhusu Linah na Amini

kiwa mwasiti ndio ametambulisha rasmi video yake hii ya Serebuka, inayosifiwa na kila mtu jijini kwa jinsi ilivyokuwa na utofauti, uliotokea kutokana na idea iliyotumika katika kufanyika kwa video hiyo kali ya serebuka, mbali na uzuri wa video hiyo mengi yameanza kuongelewa haswa kutokana na Linah akionekana kubusu picha ya aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Amini, huku watu kujiuliza ni nini haswa kinaendelea au ndio kuserebuka kwenyewe.
Linah na Amini walishawahi kuwa wapenzi, ila baada ya muda kila mmoja alikiri kuwa wamebaki kuwa marafiki wakubwa tu, huku tetesi nyingine zikisikika kuwa Linah ameshachukuliwa na mtu mwingine ambaye siyo Amini, hadi ilipoonekana katika kipande cha video hiyo mpya ya Mwasiti, na kuacha watu midomo wazi, kila mtu akijiuliza ni kweli itakuwa wamerudiana au ni Sanaa tu iliyotumika katika kufikisha ujumbe katika video hiyo mpya kali ya Mwasiti.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad