Wambura Afichua Wachezaji Mamluki Simba

MGOMBEA urais wa klabu ya Simba, Michael Wambura, amesema kuwa wachezaji wengi wa klabu hiyo ni wachezaji wa watu binafsi na siyo wa klabu kutokana na mfumo mbovu wa usajili unaoruhusu wachezaji kusajiliwa bila ridhaa ya rais wa klabu.

Wambura ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo kwenye uongozi unaomaliza muda wake, alisema utaratibu wa usajili wa klabu unatakiwa kuthibitishwa na kamati hiyo kabla ya mchezaji kuidhinishwa rasmi kuwa mchezaji wa Simba lakini hilo limekua halifanyiki.

“Kwa kawaida kamati ya utendaji ndiyo huwa inapitisha masuala ya muhimu yanayoigusa timu moja kwa moja ikiwemo usajili, sikumbuki hilo limefanyika lini lakini wachezaji wapya wamekuwa wakisajiliwa kila siku," alisema.

"Kama mjumbe wa kamati hiyo hakuna kikao chochote kilichofanyika kuhusu usajili wa wachezaji wapya, lakini pia mikataba wanayoingia wachezaji na timu imekuwa ikifanywa na watu binafsi kwa kutumia jina la timu.

“Hili linaigharimu timu sana hususani kunapokua na migogoro kwani wale wamiliki wa wachezaji huweza kuwaamuru wacheze chini ya kiwango ili kuonyesha upande fulani haufai, nadhani hilo ni moja ya mambo ya kukemea sana kwa mtu anayetaka maendeleo ya Simba.”

Katibu huyo wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania (FAT-sasa TFF) alisema ipo haja ya klabu hiyo kuwa na Idara ya Sheria itakayoshughulikia masuala ya mikataba ya wachezaji kabla ya kutumika kwenye usajili na mambo mengine yanayohusika na kisheria kwenye klabu hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad