Wambura, Kaburu Ngoma Nzito, Wakalia Kuti Kavu Uchaguzi Simba

Wagombea Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na Michael Wambura wamekalia kuti kavu kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba uliopangwa kufanyika Juni 29 mwaka huu.

Kamati ya Uchaguzi chini ya mwanasheria, Damas Ndumbaro iliwaweka kitimoto wagombea wote waliowekewa mapingamizi huku pingamizi la Kaburu likionekana kuwa ngoma nzito zaidi kwa mgombea huyo.

Kaburu aliwekewa pingamizi na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Ather Mwambeta (kadi namba 01005), ambaye alidai Kaburu akiwa Makamu Mwenyekiti alikiuka katiba ya Simba ibara ya 33 (5) na 28 (1b) kwa kushindwa kuwasilisha ripoti ya mapato na matumizi ya fedha katika mkutano mkuu wa 2010 hadi 2013 alipojiuzulu.

Kwa upande wa Wambura, ameongoza kuwa na mapingamizi mengi zaidi (matano) aliyowekewa na wanachama Swalehe Madjapa, Daniel Kamna, Said Rubeya ‘Seydou’, Ustadh Masoud na Chacha.

Akizungumza na gazeti hili jana, Wambura alisema: “Nimesikiliza mapingamizi yangu, hoja zote zilizotolewa na walioniwekea pingamizi ni zile zile za miaka yote, hakuna mpya, wote wamekuja na hoja moja ya kwenda mahakamani na mimi nimezijibu kwa hoja.”
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wambura is not satisfied bcoz atavaa viatu vya kazee ka Tabora kalikotuharibia simba ye2

    ReplyDelete
  2. Naomba kuuliza ni kwanini wanapenda kumpinga wambura kila akigombea!!!!! Jatibuninkuwa na viongozi wasomi na siyo kuwapinga kwa mkubumbo hatutakuwa na maendeleo

    ReplyDelete
  3. Wambura alivunja katiba asikimbie kivuli chake....................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Njoo mjini utajua

    ReplyDelete
  5. Simba tunajua Rais wetu ni Wambura sasa wewe unaposema ngoma nzito sijui ipi, Aveva vyeti vyake vinaonyesha utata hamuoni kama ndio ngoma ngumu kwake? Mtajiju Wambura ais wa Simba hata mtumike vipi.

    ReplyDelete
  6. wambura huna pesa kaa kando, utasajil kwa hela gani au ya rage?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad