Wapinzani Bungeni Wamkaanga Zitto

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni jana ilimlipua mbunge kutoka kambi yao, Zitto Kabwe ikimhusisha na ufisadi wa Sh119 milioni kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa).

Hii ni mara ya kwanza kwa kambi ya upinzani kumhusiaha mbunge ‘mwenzao’ na tuhuma za ufisadi tofauti na kawaida yao ya ‘kuwashughulikia’ ubadhirifu katika Serikali.

Zitto, mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema na ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), anadaiwa kuchota fedha hizo kupitia kampuni ya Leka Dutigite ambayo ina hisa nyingi katika kampuni nyingine ya Gombe Advisors Limited ambayo Zitto ni mkurugenzi wake.

Akiwasilisha maoni ya upinzani bungeni jana kuhusu makadirio na matumizi ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mwaka 2014/15, waziri kivuli wa wizara hiyo, Joseph Mbilinyi alisema Zitto hakutakiwa kuchota fedha hizo kwa kuwa anabanwa na sheria ya maadili ya viongozi wa umma.

Alisema Zitto, ambaye katika miezi ya karibuni aliingia kwenye mgogoro na uongozi wa chama chake, ni mwenyekiti wa PAC, kamati ambayo jukumu lake ni kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika wizara na mashirika ya umma, yakiwamo Tanapa na NSSF, hivyo kulikuwa na mgongano wa kimasilahi katika suala hilo.

Tuhuma za Zitto

Katika hotuba yake, Mbilinyi alisema taarifa za kibenki ambazo kambi hiyo imezipata zinaonyesha kuwa Desemba 10, 2012, Hifadhi ya Taifa ya Saadani ilihamisha Sh12 milioni kwenda katika akaunti ya kampuni ya Leka Dutigite.

“Siku moja baadaye fedha hizo zilitolewa kwa pesa taslimu kutoka kwenye akaunti hiyo. Januari 14 na Februari 7, 2013 akaunti ya Leka Dutigite iliingiziwa Sh28.6 milioni,” alisema Mbilinyi.

Sugu alisema fedha hizo ziliingizwa na mtu aitwaye Mchange na kwamba ilipofika Februari 7 zote zilikuwa zimetolewa.

Alisema Februari 28 mwaka jana, akaunti ya Leka Dutigite iliingiziwa Sh32.3 milioni kutoka NSSF na kwamba siku hiyo hiyo fedha hizo zilitolewa kwenye akaunti hiyo. Siku nne baadaye shirika hilo lilifanya malipo mengine kwenye akaunti ya Leka Dutigite.

“Ziliingizwa Sh46.6 milioni ambazo zilitolewa kutoka kwenye akaunti hiyo kwa mikupuo miwili. Katika kipindi cha miezi mitatu, kati ya Desemba 10, 2012 na Machi 4, 2013 kampuni hiyo (ya Zitto) ililipwa Sh119.9 milioni kwa utaratibu huohuo wa ingiza-toa fasta,” alisema Mbilinyi.

Alisema kati ya fedha hizo Sh12.2 milioni zililipwa na Tanapa na Sh79 milioni zililipwa na NSSF.
Tags

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kah hakuna muaminifu hapa duniani, ni mungu peke yake na mitume wake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Zitto aliposuka zengwe la uongo kuhusu mabilioni ya uswiss alitaka chadema iingie mkenge wa kumuunga mkono lakini walimstukia,wakamuacha akaogelea na kuzama mwenyewe.Maskini Zitto mbona unazidi kujimaliza mwenyewe kisiasa,yaani kwako kila siku iitwayo leo ni bora ya jana kwako?

      Delete
    2. Tulia ww huo mziki mzito sio wa kukurupuka, peke yake tu, nisawa na muunganiko wa LISU, MBOO WE, LEMA A, na nusu ya SLAA. wakiungana wote hao ndio yeye mmoja kwa uwezo.

      Delete
  2. Zitto ni fisadi wa kutosha,kapiga mamia ya mamilioni ya Usalama wa Taifa chini ya uratibu wa' zee lenye sura ngumu' steven wassira kumbe hazikumtosha,sasa kaingia kutafuna pesa za wafanyakazi.

    ReplyDelete
  3. bongo kila mwanasiasa ni fisadi tena wanaiba kwa kutumia ujuzi. mpaka wakidhurumiana ndio siri inafichuka.. lol

    ReplyDelete
  4. Mchungaji Mtikila ana kesi 14 mahakamani,Mbowe kesi 9,Lupumba kesi 4,Dr Slaa 3,Lema kesi 5,Msigwa kesi 2, Lissu 3,Lwakatare kesi 1,Machemli 1, Shibuda kesi O,Mrema kesi 0,John cheyo kesi 0 ,Zitto kesi O.Wewe Zitto ni mpinzani wa aina gani usiyekuwa hata na kesi moja ya kuku mahakamani?

    ReplyDelete
  5. Huyo sugu aache uongo wake akae ajipange na maish mapya nje ya ubunge maan 2015 hatumpi

    ReplyDelete
  6. sugu mwenyewe hana mke, sa unafikiri yupo sawasawa?, anaropoka tu kama anaimba hip hop zake za kizamani

    ReplyDelete
  7. ajipange maana hapa mbeya mjini hatujaona jipya zaid ya kuwapa viposho mbeya city

    ReplyDelete
  8. Njoo upumzike kwetu kaka maana majitu yamekuwa hayabebeki.
    Huyu ndio raisi wa kigoma bwaaaaaa,kalumanzila anakusubiri saaana!

    ReplyDelete
  9. anoy 11:55 hv kuwa mpinzanu lazima uwe na kesi? au ndo katiba za upinzani ndio zinavyosema? kwa kukurekebisha machemli ana kesi zaidi ya 1 tena za madai anadaiwa na wapiga kura wake kwa utapeli

    ReplyDelete
  10. zitto nakukubali, chadema unaogopwa kwa elimu yako n confidence..... Wakimbize sana maana hawalali ajili yako

    ReplyDelete
  11. Zitto hatishwi na kerere za mbwa, halafu kubweka kwa mbwa binadamu huwezi kuzia, wao wabweke tu, yeye bado ni zitto wala hachafuki kwa hayo, ni hila na ubaguzi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad