Wassira Awatisha Ukawa, Asema Wasiporudi Bunge la Katiba Hili Litatokea

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Stephen Wassira amewatisha wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwamba wasiporejea bungeni, kanuni zitabadilishwa na Bunge litaendelea.

Wassira alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akijibu hoja za wabunge mbalimbali akiwamo Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kuwa majadiliano ndani ya Bunge la Katiba yanakiuka Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Katika mchango wake, Mdee alisema Ukawa hawako tayari kurejea ndani ya Bunge Maalumu la Katiba Agosti, mwaka huu endapo majadiliano ya Katiba hiyo hayatajikita kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba.

Hata hivyo, Wassira akijibu kauli hiyo ya Mdee na wabunge wengine waliopaza sauti kuhusu kukiukwa kwa sheria hiyo alisema: “Kama hamrudi tutatumia kanuni zile kutafuta akidi na Bunge litaendelea.”

“Tusigeuze Bunge hili kuwa Bunge la Katiba… Bunge la Katiba lipo tena lipo kisheria…. Kuna watu wanageukageuka wanasema sheria ilivunjwa, lakini hawasemi kifungu gani kilivunjwa,” alisema Wassira.

Wassira alisema wajumbe wa Bunge la Katiba walitunga Kanuni za Bunge hilo na miongoni mwa waliokuwa walimu wa kanuni hizo alikuwa Ismail Jussa na Tundu Lissu ambao ni wajumbe wa Ukawa.

“Kanuni tuliyotunga ambayo haipingani na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ni Bunge hilo kuwa na mamlaka ya kubadili, kurekebisha, kuboresha na kadhalika,” alisema Wassira na kuongeza:
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wasira Akili mbaya,roho mbaya na Sura mbaya kama mavi ya asubuhi.

    ReplyDelete
  2. Mzee una sura mbaya kama goti la nyani?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad