Waziri Magufuli Amelidanganya Bunge

Nipo hapa nikisikiliza hotuba ya Bajeti ya wizara ya Ujenzi inayosomwa na Waziri John Magufuli. katika hotuba yake ameliambia Bunge sasa hivi kuwa UJENZI WA BARABARA YA LAMI KUANZIA TABATA DAMPO HADI KIGOGO UNAENDELEA.

Jamani mimi ni mtumiaji wa kila siku wa barabara hii ya Tabata Dampo Kigogo nikitokea Tabata Segerea kuelekea Mjini kwenye shughuli zangu. Mara ya mwisho nimepita leo hii jioni. ukweli ni kwamba WAZIRI AMELIDANGANYA BUNGE na hakuna hata dalili za kuwepo kwa ujenzi wa barabara ya lami zaidi ya kuharibika vibaya kwa barabara hiyo.

Nawaomba wabunge wa dar es salaam kusimama kidete kupinga uongo huu wa Magufuli ambao hauna faida kwa wananchi. Mnyika na Mbunge wa Kinondoni Idd Azan tafadhalini hakikisheni mnamwambia ukweli Magufuli kuwa amewadanganya wananchi na taifa lote kwa ujumba.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hana jipya huyu kilaza na digrii yake ya Bunsen burner

    ReplyDelete
  2. Magufuli amebakia kujimwagia MISIFA tu kama ndug. yake Kikwetu.

    ReplyDelete
  3. hana jipya,kawapunja wananchi wa nzega malipo ya fidia ya ardhi et kawalipa mita skwea moja kwa sh. mia na hamsini tu, huku akijua ni sh. 5000 kwa mita skwea moja,barua ya malalamiko ipo mezani kwake lakini hadi leo tunasubiria majibu yupo kimya! miezi mitano imepita sasa!kila nikienda wasaidizi wake wanadai bado hajaijibu mara yupo safari,ukiwauliza kaipata hy barua wanasema ndiyo,mbona majibu hatoi?

    ReplyDelete
  4. daah hii bajet ya mwaka huu ngoja 2one'

    ReplyDelete
  5. Kuanza kwa ujenzi kunamaanasha mengi inaweza kuwa iko kwenye stage ya upembuzi...wewe ndo hujaelewa

    ReplyDelete
  6. Wewe hujui maaayaujenzi kuendelea?au magufuli babuyako?huyo magufuli muongo sana kasema barbr yamikumihadi kigogo darajani ujenzi unaendelea kumnbe hewa,j
    kaleta mkandarasi WA daraja la mto mzimuni,daraja limepinda,majiyanaeda makaziya watu,katoa maagizolivunjwe mpakaleo miaka zaidiya3 hakunakinachoendelea

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad