Waziri wa Nishati na Madini, Prof.Muhongo Akaliwa Kooni ang`oke!

Moto umeendelea kumbabua Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kutokana na tuhuma za kuwapendelea wageni na kuwakandamiza Watanzania.

Waziri huyo amekuwa akilalamikiwa na Watanzania wazawa kutokana na kauli zake za kuwatukana, kuwabeza na kuwadhalilisha akidai kuwa hawana uwezo wa kushiriki katika biashara ya kuvuna gesi asilia na mafuta kutokana na kutokuwa na fedha kama mitaji.

Aidha, Profesa Muhongo amekuwa akisema kuwa Watanzania wana uwezo wa kuuza juisi na kukaanga chips na kwamba wanaolalamika wakitaka kupewa upendeleo ili kunufaika na rasilimali za taifa ni wezi na wababaishaji.

Safari hii Rais Jakaya Kikwete ameombwa kumuondoa Profesa Muhongo katika Wizara ya Nishati na Madini kwa madai kuwa analidhalilisha taifa kutokana na vitendo vyake vya kugawa madini kwa wageni na kuwaondoa mamilioni ya wazawa kwenye uchimbaji dhahabu na madini mengine nchini.

Profesa Muhongo amelalamikiwa kwamba amepandisha gharama za ushuru wa uchimbaji wa madini kutoka Dola Kimarekani 100 hadi 10,000.

Tamko hilo lilitolewa mjini Dodoma na vijana 138 ambao ni wachimbaji wa madini kutoka mikoa ya Singida, Tabora Simiyu, Shinyanga, Chunya (Mbeya), Tanga, Mara na Tunduru (Ruvuma).

Wachimbaji hao walisema kwamba tangu Muhongo ateuliwe ameigeuza wizara kuwa mali binafsi kutokana na kuwabambikia wachimbaji madini ushuru mkubwa wa gharama za leseni.

Walisema kuwa waziri huyo ameuongeza kutoka Dola 100 hadi 10,000 kwa mwaka na kuhoji kama ana nia ya dhati ya kuwawezesha wazawa kunufaika na uchimbaji.

Vijana hao walisema katika tamko lao kwamba hatua ya waziri Muhongo ina lengo la kuwafanya waendelee kuwa masikini na kuapa kwamba hawatakubali na kwamba wanamuomba Rais kikwete amuondoe katika wizara hiyo.

Wachimjaji hao wamesema kwamba ikiwa Profesa Muhongo hataondolewa katika wizara hiyo wataachukua hatua ikiwamo kuandamana kushinikiza ajiondoe mwenyewe.

Wamesema kuwa Waziri Muhongo hafai kuwa kiongozi kutokana na kauli zake zisizo na staha na kusema uongo.

Aidha, walikosoa hatua yake ya kuwapeleka nje ya nchi baadhi ya viongozi wa dini kujifunza jinsi nchi nyingine zinavyovuna gesi asilia kuwa haina lengo zuri kwa kuwa waliotakiwa kupelekwa ni wafanyabiashara.

Naye Prof Chris Berge kutoka Norway akizungumza katika kongamano hilo alisema kuwa sera zinazolinda wazawa ni muhimu sana kuondoa umasikini kwa jamii kinyume na fikra za viongozi wingi wa Kiafrika ambao wanaamini kuwa uwekezaji kutoka Ulaya ndiyo utakaomaliza umasikini.

Profesa David Green na Dk. Ahmed Mahze kutoka Australia na Ujerumani walisema ni lazima Bara la Afrika liwe na ujasiri wa kupambana na rushwa, na kutoa mfano wa Dk. Reginald Mengi kuwa ni mfanyabiashara pekee aliyethubutu kukemea na kulaani rushwa hadharani.

Kongamano hili la siku mbili linaloshirikisha wachimba madini na viongozi wa dini nchini, lilifadhiliwa na mashirika ya kidini ya kujitolea kupambanana na rushwa Afrika kwa kutumia raslimali zilizopo yakiwamo madini na kilimo.

Washiriki waliazimia kuitaka serikali kuacha utaratibu wa kuwabugudhi wachimbaji wadogo wadogo kote nchini baadala yake iwashirikishe yanapogundulika madini kwa kuwa ndiyo watakaokuwa wachimbaji wakubwa siku zijazo.

Chanzo: Nipashe
Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. duuu kweli atumtaki

    ReplyDelete
  2. atoke tu atumtaki, umeme umepanda sana, jamaa ana dharau anajali tumbo lake na c wananchi wa hali ya chini

    ReplyDelete
  3. sana anasura ya kukela sana sijui jk anawatoaga wapi watu km hawa anajisikia yan ni shida

    ReplyDelete
  4. sura baya na roho chafu, imebaki wananchi tuandamane tumechoka uongoz huu,

    ReplyDelete
  5. Ila manenoyake mengingine nikweli WA tz wengi niwababaishaji,mfano wakipewakaziwakandarasi wannje wakandarasi wahapa wanalalamika wakipewa wao naukiwapa advanc wanakimbia miradi he jetuwafanyeje?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha usenge wewe unawafagilia hao mabwana zako mara ngapi kampuni za nje zinakimbia kaa chini uulize!

      Delete
  6. we wa juu apo acha kumtetea jamaa atumtaki anapandisha sana umeme mkiandamana mtuambie nasisi tujiunge pmj

    ReplyDelete
  7. wawekezaji hawajali maslahi ya wazawa wala hawana uruma na mtu wao kuchuma aslimia 75 nyie na serikali mnabakiwa na 25,je hizi 25 zitatutosha sana sana zinishia serikalini.haya ni maoni yangu sijui wenzangu mnasemaje?

    ReplyDelete
  8. kumbuka mtu yeyote akiitwa pro hafai kuwa kiongozi wao kazi yao kubwa ni wavumbuzi,wanareaseach na walimu sio kuongoza wizara au nchi ndiyo shule wamesoma kiukweli sijui tatizo liko wapi?

    ReplyDelete
  9. huyu muheshimiwa me ninachojua ni mtu wa kazi na hana siasa na huwa anasema vitu vya ukweli na toka aingie yy pale wizara imetulia ila cc hatupendi kuambiwa ukweli. enyi wachimbaji wadogo jiungeni pamoja na kukusanya mtaji mkubwa mtaweza tu kushinda

    ReplyDelete
  10. hii wizara ilikuwa kila ukiamka asubuhi lazima usikie kituko lkn toka aingie huyu mambo yanasonga mbele na kwa uhakika kuhusu umeme tuelewe kwamba hapandishi waziri ni hali halisi kama gharama za uzalishaji ikiwemo wafanyakazi, mafuta nk

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad