Wema Sepetu na Aunt Ezekiel Wamwingiza JB Mkenge

IMEKULA kwake! Wauza nyago kwenye sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson wamemuingiza mkenge staa mwenzao, kaka mkubwa Jacob Steven ‘JB’ baada kukubali mwaliko kisha kumkatalia dakika za mwisho.

Habari za ndani zilidadavua kwamba JB na wasanii hao walitakiwa kusafiri kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya kujifunza utamaduni wa huko ambapo walipelekwa na uongozi wa Ukumbi wa Princess Cassino uliopo Posta jijini Dar.

Katika hali ya kushangaza, uongozi huo ukiwa tayari umeshawakatia tiketi za daraja la kwanza (first class) zinazogharimu kama dola elfu moja (zaidi ya Sh. milioni 1.6) kila mmoja na baadhi ya wasanii kama Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ na Amri Athuman ‘Mzee Majuto’, Wema na Aunt Ezekiel walikataa siku moja kabla ya safari.

Chanzo chetu makini kilipenyeza habari kuwa, Wema na Aunt walichomoa safari hiyo baada ya kuhisi haikuwa na maslahi kwao na walivyopeleka maombi yao ya kimaslahi kwa JB, aliwaambia ni safari ya kujifurahisha na hakuna fedha yoyote watakayopata.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Aunt ambaye alikiri kuchomoa safari hiyo baada ya kushindwana kimaslahi.

“Unajua ile ni kwenda kutangaza biashara ya mtu kwa hiyo sisi tuliwatajia kiasi cha fedha ambacho tulikitaka kulipwa lakini tulishindwana ndiyo maana tukakataa kusafiri maana hatuwezi kufanya kitu ambacho hakina maslahi kwetu na kwenda kuwafaidisha wengine,” alifunguka Aunt.

Naye Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ aliilaani safari hiyo na kusema kwamba JB ni mnafiki kwani aliwachagua wasanii wachache kwa upendeleo ambao baadhi yao wamemwangusha kwa kutokwenda.

“Ukweli nimegundua JB ni mbinafsi, nilikuwa naambiwa lakini nikawa namtetea, sasa nimeamini kwamba hafai akirudi lazima nitamuita, nitazungumza naye kwa nini aliamua kufanya hivyo wakati kila kitu kinapotokea iwe safari au vitu vingine huwa sisi Bongo Movie Unity tunashirikishana lakini kwa hili ameona afanye mwenyewe,” alisema Steve Nyerere.
GPL

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wapi wewe steve, we sema umekosa fursa au ulitaka muuende bongo movie wenyewe na hilo group lenu, hujapenda majito kukwea pipa sio? huyo wema anamambo yake kibao na diamond wake kwenda kwake ingeshindikana na wala si maslahi aunt fata mkumbo tuuu huyo.

    ReplyDelete
  2. HK kijitukifupi kinamatatizo HK kimekaa kinjaanjaa tu.acha uzushi Wako uambiwe wewe nani ili uende wewe.nawewe jb hukuwaeleza watu mapema mantiki yahiyo safari yenu ungeweka wazi kabla.next time usirudie

    ReplyDelete
  3. aibu bongo movie yote hamjielew

    ReplyDelete
  4. HAO WASANII WALIOKATAA KWENDA HUKO WAKO SAHIHI,HIVI INAWEZEKENAJE MKATIWE TIKETI TU,YA KWENDA HUKO,MSIPEWE HELA YA MATUMIZI,NA NAWAUNGA MKONO,YAANI MKATEMBEE TU ,HAAA JAMANI MSIWAFANYIE HIVYO WENZENU,

    ReplyDelete
  5. jb ni boya na ubonge wake, yan ukawatembeze wenzio uturuki bila posho.... Stupid guy

    ReplyDelete
  6. Huko uturuki kwenyewe kinanuka kila leo watu wanachapana!ndio uwapeleke wenzio bure?

    ReplyDelete
  7. Wema awezi ku shituka kwenda ku tali uturuki? wakati uwa anaenda zake USA, CHINA, ENGLAND na yuko bus na D7 kwenda zawo Kwenye BET AWARD ku met na JAY-Z,BEONCE, RIHANA...

    ReplyDelete
  8. JAY B kweli noma unataka kuwa peleka wenzio uturuki bila posho ..,WEMa na Unty muko powa

    ReplyDelete
  9. Wema..,,kutalii bure ? jay be stupid

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad