Werema Kuomba Msamaha Pekee Hakutoshi, Aachie Ngazi!

Kuomba msamaha bungeni kwa Werema hakutoshi. Wadhifa alionao ni mkubwa sana kiasi ambacho kuomba kwake msamaha ni kama "machozi ya mamba" analia huku anakumeza.
Watanzania kwa kauli hiyo ya Werema bungeni hatuna imani nae tena na hususan Wazanzibari, hawatokuwa na imani tena na Werema.
Kwa kuwa kakiri mwenyewe kuwa ana kinyongo, ina maana kuwa hata iweje hawezi yeye kugeuka Yesu Aleyhi Salaam au Muhammad Swalla Llahu Aleyhi Wasalaam, kwa kauli yake mwenyewe wakati wa kuomba msamaha, kwa hilo inabidi aachie ngazi kwa hiyari yake na akikataa kwa hiyari yake basi kwa kushinikizwa.

Watanzania tuungane kuutokomeza huu ubaguzi. Wabunge wote wapenda haki na wale wasioupenda ubaguzi washirikiane kushinikiza Werema aachie ngazi.

Asamehewe pale tu atakapoachia ngazi. Wadhifa alionao haumtaki, haumfai wala haiyumkini awekwe mtu aliyekiri kosa la ubaguzi hata chembe, akiwa madarakani au nje ya madaraka. Kumuacha Werema kuendelea na wadhifa huo ni kosa kubwa zaidi. Waswahili wanasema "akumulikae mchana usiku atakuchoma".

Yeye, kama mwanasheria anatambuwa kabisa, kukiri kosa na kuliombea msamaha hakutengui adhabu ya hilo kosa kisheria. Kosa la ubaguzi kwa mtu mwenye wadhifa kama wake ni kuachia ngazi tu. Kuomba kwake msamaha hakumtoi nyongo wala kinyongo, kama ni nyongo inabaki pale-pale na kama kinyongo kiko pale-pale.

Nawasilisha.

Chanzo:

Kitendo hicho cha Wazanzibar kutusiwa, kutukanwa na kubaguliwa hadharani bungeni, kimefanywa na Mwanasheria Mkuu, Frederick Werema akibebwa na kiti ambacho wakati maneno hayo ya utusi na ubaguzi yakitamkwa, kilikuwa kimya.

Kiti hakikuishia kukalia kimya tu kitendo hicho cha aibu na fedheha ambacho kinazidi kuongeza ufa wa Muundo wa Muungano wa Serikali Mbili, bali pia amedhihirisha udhaifu mkubwa alionao katika uongozi, pale alipozuia muongozo wa Mbunge Rajab Mohamed Mbarouk, ambaye alitaka hatua zichukuliwe.

Ilikuwa hivi; Mbunge Habib Mohamed Mnyaa, alitaka Waziri wa Katiba na Sheria alieleze bunge kwa nini wizara hiyo imekuwa ikivunja sheria wazi wazi katika mchakato wa Bunge Maalum la Katiba...

Akasimama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Werema katika hali inayoonesha kiburi, kulewa madaraka, kutojua anachokizungumza au kujikuta akitoa yaliyomjaa moyoni, akamjibu akimwambia "hayo kaulize huko kwenu Zanzibar...hapa kwetu...".

Karudia kauli hiyo akim- address Mnyaa kwamba "hayo kaulize huko kwenu Zanzibar...ukija hapa kwetu huwezi kuuliza hayo..." mara kadhaa, huku kiti kikiwa kimya, hali ambayo imedhihirisha kuwa kilikuwa kinabariki ubaguzi ule.
By  FaizaFoxy, Via JF
Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. jiuzulu mkurya wewe, ndo solution

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe usitaje makabila ya watu acha ushamba, tena wewe ndo unaonekana mbaguzi,

      Delete
  2. wapo wengi kama yy..lkn yy ameshindwa kujizuia

    ReplyDelete
  3. Mi naona mambo ya kujiuzulu hayasaidii mbona kasheki amejiuzuru lakini tembo wanauawa kama kuku hii ndi tz

    ReplyDelete
  4. Mura hakuna kujiuzulu, wazenji inabidi wapewe makavu live, Muungano mpaka waje kuungania kwenye bunge letu la bara?.wanaserikali yao rais wao mbona hamjasema hapo muungano hakuna mtu akisemaukweli aaah anavunja muungano kwendeni zenu huko na unafiki wenu.

    ReplyDelete
  5. tukipata watu kama nyinyi ndio ss wazanzibar tunafurah cz mnarahisisha kupata nchi yetu....tuachieni nchi yetu tushachokaaaaaaaaaaaaa yakheeeeeee

    ReplyDelete
  6. Werema sio mtu!

    ReplyDelete
  7. Hayo nimawazo yke werema ww je?

    ReplyDelete
  8. Warema ajiuzuru; kwakosa ngani???? Kumueleza mwana-ukawa ukweli ni kosa? Lazima wakemewe vinginevyo ukweli utapotoshwa kupita uongo kupitia itikadi ya "UKAWA-DISGUISELISM"

    ReplyDelete
    Replies
    1. we kuma kweli,ukweli gan unaoujua ww?

      Delete
  9. Umoja no nguvu jamani .ubaguzi so ishu .

    ReplyDelete
  10. Who knows,may be he was telling the truth!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad