Wolper Apiga Mweleka kwenye Kibao Kata.Gambe Zamzidi


Mbovumbovu za staa! Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe anadaiwa kuwa tilalila na kujikuta akipiga mwereka kwenye shughuli ya kibao kata cha mwigizaji mwenzake, Vanita Omary.

Kwa mujibu wa ‘shushushu’ wetu aliyekuwa ndani ya nyumba, tukio hilo lilijiri kwenye Ukumbi wa PG Hall (zamani FM Club), Kinondoni jijini Dar ambapo mastaa kibao walihudhuria.

Ndani ya kibao kata hicho, Wolper alicharuka kipombepombe kwa kucheza ovyo na kukimbiakimbia akiwa tilalila.

Katika kukimbia huko, ndipo akapiga mwereka na kuanguka huku akijaribu kusimama kwa kuchechemea.
Baadhi ya wageni waalikwa walibaki wakimshangaa na kusema kuwa hapendezi akinywa pombe kwani ustaarabu wote unapotea.

Mbali na pombe pia alikuwa kivutio kwa staili ya ukataji wake wa mauno akiwa na kivazi kilichoacha nje mapaja yake akiwa na rafiki yake aliyetajwa kwa jina moja la Vivi.

Katika hatua nyingine, Vanita alijikuta akiangua kilio baada ya wapiga ngoma wa kibao kata ‘kuwa feki’ na kushindwa kufanya kazi kama walivyoahidi.
Kutokana na hilo, baadhi ya mastaa kama Aunt Ezekiel na Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ waligoma kucheza na kukizomea kibao kata hicho ambacho kililetwa na MC (jina linahifadhiwa) akidai kuwa amewatoa Bagamoyo na wana ufundi wa hali ya juu

Mwisho wa shughuli, MC huyo alimvaa Vanita akitaka alipwe pamoja na kwamba wapiga ngoma wa kibao kata hicho walishindwa kazi hivyo kukaibuka mtiti wa aina yake huku kila mtu akitimua zake.
Stori:  Hamida Hassan na Imelda Mtema

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ovyo ukimuona utaona mwanamke mstaarabu na kujiheshimu Kumbe Malaya mkubwa unafanya mchezo bangi na pombe utakufaaaa!

    ReplyDelete
  2. Akomee gambe hana ustaarabu wowote Ana act tu

    ReplyDelete
  3. kumbe ni msagaji kweli...alikuwa anapagawa kusikia harufu yavikuma,,mpaka mweleka

    ReplyDelete
  4. Wewe nana sikuwezi kwa kwel

    ReplyDelete
  5. nana noma nipe namba yako

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad